Home » » Ndugu wasusa kuchukua maiti ya mtuhumiwa aliyekamatwa na nyara za Serikali

Ndugu wasusa kuchukua maiti ya mtuhumiwa aliyekamatwa na nyara za Serikali


Na Walter Mguluchuma, Mpanda-Katavi yetu
Mwili wa mtuhumiwa aliyekamatwa na nyara za serikali umeendela kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Mpanda kwa muda wa  siku tano sasa  kufuatia ndugu wa marehemu kugoma kuuchukua kwa ajili ya mazishi kwa madai kuwa marehemu alikufa kutokana na kipigo alichokipata kutoka kwa askari wa hifadhi ya katavi na polisi.
Mke wa marehemu aitwaye Elias Joel alisema siku hiyo ya tukio mumewe Joel Lucas (55) mkazi wa kijiji cha Kanoge makazi ya Katumba alikamatwa na askari wa hifadhi ya wanyama ya katavi na polisi na kisha walimpa mateso makali katika kichaka kilichojirani na nyumba yake.
Alisema tukio hilo lilitokea Juni 30, mwaka huu majira ya saa 8:00 usiku nyumbani kwake alikokuwa akiishi
Elisia alieleza siku hiyo akiwa amelala na mumewe ambaye nimarehemu kwa sasa walipigiwa hodi ya kuwataka wafungue mlango na ndipo waliposhauriana watoke nje na walipotoka nje alidai alimwona mtu mmoja akiwa na baiskel akiwa amesimama nyuma amefunga kifurushi.
Alisema wakatai wanamshangaa mtu huyo mbwa waliokuwa jirani walikuwa wakifoka sana na  kumfanya mumewe afuatilie kuna nini huku ndipo alipowakuta askari wa jeshi la polisi wakiwa na askari wa Hifadhi ya Katavi waliomuweka chini ya ulinzi kuanzia muda huo.
Baada ya kumuweka chini ya ulinzi walitafuta majirani kwa ajili ya kupekuwa nyumba ya mtuhumiwa huyo ambaye walikuwa wakimtilia shaka kujihusisha na ujangiri haramu wa meno ya tembo.
Zoezi la kupekua nyumba liliendelea na walipomaliza nyumba ya mbele walihamia nyumba ya uani ambapo waliingia kwenye chumba cha mtoto wao aitwaye Hajangimana Joel (16) na kukuta ndani kuna meno mawili ya tembo  na walipomuuliza aliwajibu kuna mtu aliyekuwa amesimama hapo nje na baiskel ndiyo ameyatupia hapo mtu ambaye familia hiyo walidai hawamfahamu.
Alisema ndipo askari polisi na hifadhi ya katavi walipo wafunga pingu marehemu na mwanae na kisha kumwamuru mama huyo awakokee moto kwani wanalala hapo kwake.
Ilipofikia alfajiri walimuomba mama mwenye nyumba awapatie majembe na panga ambayo waliyatumia kwa ajili ya kufukua maeneo ya nyumba yao kwa lengo la kutafuta silaha
Alisema baada ya kuikosa silaha walimchukua mwanae Hajangimana na kwenda nae kichakani huku wakimwacha baba yake ndani ya gari la hifadhi ya Katavi
Baada ya muda walimrudisha na kisha  walimchukua mumewe na kumpeleka katika kichaka hari ambayo ilimfanya yeye afuate kwa nyuma kwa kujifichaficha na ndipo alipomwona mumewe akiwa amening’inizwa juu ya mti akiwa amefungwa pingu na huku akipokea kichapo kutoka kwa askari hao zoezi hilo ambalo lilichukua muda mrefu
Alisema baada ya kumwona ameisha ishiwa nguvu alidai waliamua kumshusha  na kumpakea kwenye gari na men ohayo mawili ya Tembo akiwa na mwanaye na kupelekwa kituo cha polisi cha Mpanda ambapo marehemu alifariki muda mfupi baada ya kufikishwa katika hospital ya wilaya yam panda
Mdogo wa marehemu Ally Kazinge alisema wao kama ndugu wa marehemu hawako tayari kuuchukua mwili wa marehemu mpaka hapo uchunguzi wa kina zaidi utakapofanyika wa kidaktari.
Alisema hawa taridhika na taarifa iliyotolewa ya kidaktari kuwa ndugu yao amefariki kutokana na shinikizo la damu.
Alieleza miongoni mwa ndugu wa marehemu walioukagua mwili wa marehemu  alikuwa ni yeye na alikuta mwili huo ukiwa na majeraha mikononi na miguuni wakati ukiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa katavi Dhahiri Kidavashri alieleza kuwa toka juzi walikubaliana na ndugu wa marehemu wauchukue mwili huo kwa ajiri ya mazishi wakati jeshi lake likiwa linaendelea na uchunguzi
Alieleza kushangazwa na ndugu hao kuendelea kuchukua mwili wa marehemu wakati tayari wameshakubaliana mwili huo uchukuliwe na ndugu kwa ajiri ya mazishi.
Alisema tayari polisi wamefungua jerada la uchunguzi kuhusiana na malalamiko hayo na ametuma askari wake waende kwenye eneo hilo kwa uchunguzi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa