Home » » ZAIDI YA WATU 200 HAWANA MAKAZI YA KUISHI KATIKA KIJIJI CHA ITOPA

ZAIDI YA WATU 200 HAWANA MAKAZI YA KUISHI KATIKA KIJIJI CHA ITOPA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 




Na    Walter   Mguluchuma.
     Katavi.

ZAIDI ya kaya 200 katika kijiji  cha Ipota katika kata ya Ikuba katika
wilaya ya Mlele mkoani Mlele  hawana makazi ya kuishi  baada ya nyumba
zao kuteketezwa kwa moto  na askari wa Shirika la hifadhi za  mbuga za
Taifa (Tanapa)  na askari polisi kwa madai kuwa sio makazi rasmi.

Tukio  hilo la lilizua  taharuki  kubwa kwa  wakazi  wa  kijiji hicho
ambapo  wa siku  mbili  mfululiozo kaya hizo  ,  wakiwemo watoto ,
wanawake na wajawazito wanalazimika kulala chini ya miti cha huku
wakinyeshewa na mvua za masika . .

Inadaiwa kuwa askari wa  Tanapa na askari polisi  kutoka kituo cha
polisi cha Kibaoni katika wilaya ya Mlele waliteketeza nyumba za
wakazi hao kwa moto  juzi .

Kaimu  Mwenyekiti  wa  kijiji  cha Ipota,   Soguta   Masanja   Maduhu
akizungumza na waandishi wa habari   waliotembelea    hapo   kiicho
jana  alisema  kaya   210ahazina  makazi ya kuishi baada ya nyumba zao
kuteketezwa kwa  moto  na  askari hao

“  Kaya zipatazo  210  hazina makazi  ya kuishi baada ya nyumba zao
kuchomwa  moto na askari wa Tanapa na  askari polisi kutoka  kituo cha
polisi kilichopo katika kijiji  wilayani hapa (Mlele) na kusababishwa
kaya hizo  kujibanza chini ya miti usiku kucha wakinyeshewa na mvua”
alisisitiza Masanja..

 Akisimulia  tukio  hilo , Masanja   alieleza  kuwa  askari  hao
walifika  kijijini  humo juzi kwa kustukiza na  kuteketeza nyumba
hizo kwa kuzichoma moto  zoezi  lililofanyika  kwa siku mbili
mfululizo na kusababisha taharuki kubwa kwa wakazi hao .

“Kaya hizo zimepata mateso makubwa  licha ya kuchomewa nyumba zao
bado askari hao  waliwapiga  wakazi  hao ….hawakuwa na huruma  kabisa
kwani waliwapiga  watoto , wanawake ,  wajawazito na wagonjwa”
alieleza.

 Alisema  kumekuwepo  na  mgogoro  mipaka ya makazi    baina  ya
TANAPA  na  wakazi wa kijiji  hicho  na   Hifadhi  ya  Taifa  ya
Katavi  na eneo tengefu  la kijiji na uhifadhi wa misitu na wanayama
pori  “Wildlife Management Area”  (WMA) kwa muda mrefu  sasa .

Alifafanua kuwa  nyumba hizo zilizoteketezwa  kwa moto zinadaiwa na
Tanapa  kujengwa  ndani ya   Hifadhi ya Taifa ya   Katavi.

“Ukweli  ni kwamba nyumba hizo  zilijengwa  mita   800  kutoka
Hifadhi ya Taifa ya   Katavi kwani  utaratibu  na   sheria zilizopo ,
 wananchi  wanatakiwa kuwa  kujenga   makazi   yao  umbali wa mita 500
 nje  ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi  na  mita   300  nje  ya   WMA  na
 wakazi hao walifanya hivyo “ alisisitiza ..

  Aliiomba uongozi wa  serikali  ya mkoa wa  Katavi  wafike kijijini
hapo ili kupima   mipaka ya  kutoka  kwenye  Hifadhi ya Taifa ya
Katavi     hadi    kwenye  makazi  ya  kijiji  hicho  ili   ndipo
ukweli ujulikana kwa kuwa  wao   wana  uhakika  eneo hilo  wanalo ishi
liko nje ya hifadhi hiyo .

  Kwa  upande  wake   Joseph  Kalubwa  alisema  mipaka
inayotenganisha hifadhi  hiyo na kijiji hicho  ni ya asili .

Nae mkazi  wa kijiji  hicho ,Samwel   Kisinja alidai familia yake
yenye watu wapatao 32tangu juzi  wamelazimika   chini  ya  miti  usiku
kucha baada ya  makazi  yao  kuteketezwa kwa  moto na askari  hao ..

  Mkazi mwingine ,  Maria    Mchelu   alisema  mbali ya  kuchomewa  na
  nyumba  yake  pia   askari  hao  waliteketeza kwa moto   magunia
yake matatu .

Hadija   Madilisha aliiomba  Serikali  iingilie kati kunusuru  maisha
yao  huu wa   mvua  za  masikaambazo zimeanza   kunyesha  mkoani humo
.

Nae  Deus  Kuhanda   alisema wakazi  hao  wameishi kwenye  kijiji
hicho  kwa zaidi ya miaka 20
Mbunge wa  Jimbo  lao  la  Kavuu   Dk   Pudensiano  Kikwembe  alisema kuwa taarifa za kuchomewa   nyumba  kwa  wananchi  hao  amezipata  akiwa   Bungeni   Mkoani  Dodoma  hivyo  anawasiliano na  uongozi wa  Serikali wa  Mkoa  wa  Katavi ili  kuweza    kujua   ufumbuzi wa   tatizo  hilo la  wananchi na hasa kwa kutambua  kwamba  kipindi  hiki ni  cha  masika.



0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa