Home » » HOT: KESI YA MASHA NA VIONGOZI SITA WA CHADEMA YA KUINGIA KWENYE MAKAZI YA WAKIMBIZI BILA KIBALI UPANDE WA MASHITAKA KUFUNGA USHAHIDI LEO

HOT: KESI YA MASHA NA VIONGOZI SITA WA CHADEMA YA KUINGIA KWENYE MAKAZI YA WAKIMBIZI BILA KIBALI UPANDE WA MASHITAKA KUFUNGA USHAHIDI LEO



  Na   Walter   Mguluchuma .
     Katavi .katavi yetu blog
Kesi  inayo mkabili  aliyekuwa   Waziri wa   Mambo ya   ndani  ya Nchi   Lawrence  Masha  akiwa  na   viongozi   sita  wa   Chama  cha  Demokrasia  na  Maendeleo    CHADEMA  waliofikishwa   katika   Mahakama   ya   Wilaya  ya   Mpanda   kwa  tuhuma  za  kufanya  mkutano wa  hadhara  na   kuingia  bila  katika   makazi  ya  Wakimbizi  ya  Katumba  Wilayani  Mlele   Mkoa wa  Katavi  jana iliendelea kusikilizwa na  leo itaendelea  ambapo  upande wa  mashitaka  leo  umepanga kufunga   kuwakilisha  ushahidi wake .

  Kesi   hiyo  inasikilizwa  na   Hakimu   Mkazi wa   Mfawidhi  wa    Mahakama  ya  Wilaya  ya   Mpanda   Chiganga  Ntengwa  ambapo  Masha  na  wenzake  wanatetewa  na   wakili   Abelti  Msando  kutoka   Deres  salaam.

  Masha   na  na  watuhumiwa wenzake  sita  walifikishwa   Mahakamani  kwa  mara  ya kwanza Oktoba  16  mwaka  jana  huku  wakiwa  chini ya ulinzi   mkali  wa  polisi  waliokuwa  na   bunduki  na    mabomu ya  machozi   na  kusomewa   mashitaka   na   mwanasheria wa  Serikali  Mkoa  wa  Katavi    Lungano   Mwasubila.

Watuhumiwa  wengine  kwenye  kesi  hiyo    aliyekuwa  mgombea   ubunge   chadema   wa  Jimbo  la   Nsimbo   Gerald   Kitabu, Abrahamu  Mapunda   mwenyekiti wa   Chadema  wa   Wilaya  ya  Mpanda ,   Franco   Misigalo   katibu wa  Bavicha    Mkoa  wa  Katavi ,   Stansilaus   Kaswele   Mwenyekiti   Chadema    jimbo  la  Nsimbo  na   Lameck  Costantino     katibu  wa  Chadema  jimbo  la   Nsimbo .
Masha  ambae    ni   mshitakiwa  wa kwanza   wanadaiwa  kuwa  Oktoba   19  mwaka   jana  majira ya saa  saba  mchana  wote  kwa  pamoja  walitenda  kosa     hilo   katika  makazi ya   wakimbizi  ya  Katumba .
 Washitaki katika  kesi  hiyo  inayoendelea   kusililizwa  na  kuvutia   hisia  za  watu  wengi wa   Manispaa ya  Mpanda  na   Mkoa wa   Katavi  wanakabiliwa  na  tuhuma  za  mashitaka  matatu .

Shitaka  la   kwanza  ni  lakuingia   ndani ya   makazi ya  wakimbizi  bila  kibali   cha   mkuu wa   makazi ya  Katumba  na   shitaka  la  pili kuingia  ndani ya  makazi ya  wakimbizi   bila  kibali  na  kufanya  mkutano wa   hadhara   na  shitaka   la  tatu  kuingia  kwenye  makazi ya  wakimbizi  bila  kibali  cha   Waziri wa  mambo ya   ndani  ya  Nchi.

Upande  wa  mashitaka  jana  uliendelea  kutowa  ushahidi wake na  kesi  hiyo  imepangwa  kuendelea   hapo  leo   ambapo   upande  mashitaka   utakuwa  unafunga   towa  ushahidi  wake .
Masha   na  washitakiwa   wanzake   ambao  wote  walikuwepo   Mahakamani  wanaendelea  kuwa   nje  ya   mdhamana    baada  ya   kutimiza   masharti ya    mdhamana   toka   hapo   awali  walipofikishwa  mahakamani kwa  mara  ya  kwanza

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa