Home » » MCHUNGAJI WA KANISA AKAMATWA NA MENO 11 YA TEMBO YENYE THAMANI YA MILIONI 90 AKIWA AMEHIFADHI KANISANI

MCHUNGAJI WA KANISA AKAMATWA NA MENO 11 YA TEMBO YENYE THAMANI YA MILIONI 90 AKIWA AMEHIFADHI KANISANI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


   

 Na  Walter  Mguluchuma
   Katavi yetu Blog
Jeshi  la  Polisi  Mkoani  Katavi kwa  kushirikiana  na  Askari wa  Tanapa wa  Hifadhi ya   wanyama ya  Katavi  wame wamemkamata  mchungaji wa  Kanisa  la   Moroviani  Kata ya   Usevya  Tarafa ya  Mpimbwe  Wilaya ya  Mlele  akiwa  na  mtu mmoja  ambao  wajina  yao  yamehifadhiwa wakiwa na  meno ya  tembo 11 yenye  thamani ya  shilingi  milioni  90 wakiwa  wameyahifadhi  ndani ya  Kanisa.
  Kaimu   Kamanda wa  Polisi  wa  Mkoa  wa  Katavi  Damas    Nyanda  aliwaambia  waandishi  wa  Habari  jana  ofisini  kwake  kuwa  watuhumiwa  hao   walikamatwa  juzi  majira ya saa  mbili  na  nusu   katika Kanisa  la  Moroviani  ililoko katika  Kijiji  cha  Usevya.
  Alisema  Mchungaji huyo wa  Kanisa  la  Moroviani  akiwa  na  mwenzake   mmoja  ambao  majina  yao  yamehifadhi  kwa  sababu za kiupelelezi  walikamatwa kufuatia  taarifa zilizolifikia  Jeshi la  Polisi  na    kwa  Askari wa  Hifadhi ya  Taifa ya   Katavi  kuwa  watu hao wanajihisisha   na  biashara  hara  haramu ya  meno ya  Tembo  na  wamekuwa wakiyahifadhi  ndani ya Kanisa.
Baada  ya  taarifa hizo  polisi na  Tanapa  walianza  kufanya  uchunguzi kuhusiana  na  taarifa  hizo walizozita  kutoka  kwa  Raia   wema hukusiana  na  tuhuma za  biashara  hiyo  haramu ya  meno ya  Tembo.
Kaimu  Kamanda   Nyanda  alieleza  ndipo  jeshi  la  Polisi kwa  kushirikiana  na  Askari wa  Tanapa walipoweza  kufika  katika   Kanisa  la  Moroviani  Usevya  na  kufanya   upekuzi  ndani ya  Kanisa  hilo.
Katika  upekuzi huo waliweza  kukamata  meno ya  Tembo  vipande  11  yenye  uzito wa  kilogramu 20.3 yenyethamani ya  shilingi Milioni 90 yakiwa  yamehifadhiwa  ndani ya  tenga la kubebea mizigo yakiwa  yamehifadhiwa  ndani ya  Kanisa  la  Moroviani  Usevya lililokuwa  likiongozwa na  mchungaji  huyo  anaeshikiliwa  na  Polisi.
  Kaimu  Kamanda   wa  Polisi wa  Mkoa  wa  Katavi  alisema  katika   matukio  mengine  mawili  tofauti  yaliotokea  Mei   8  majira  ya saa mbili  usiku   huko   Katika  maeneo ya   Mgolokani  Kata  ya  Sitarike  Tarafa  ya  Nsimbo  Wilaya  ya  Mlele  Polisi  kwa  kushirikiana  na  Askari wa  Hifadhi ya  Katavi walimkamata  mtu  mmoja  ambae  jina  lake  limehifadhiwa  akiwa  na  jino  moja  la  Tembo ..
Kwa  mujibu wa  Nyanda  mtuhumiwa  huyo  alikamatwa   baada ya  Askari  kufanya  upekuzi  ndani  ya  nyumba  yake   mtuhumiwa  na  ndipo walipo weza  kukamatwa na jino  moja  la  Tembo  likiwa  limefifadhiwa  ndani ya  nyumba  yake .
 Tukio  la  pili  lilitokea  siku  hiyo  hiyo  katika  maeneo ya   Mgolokani  Kata  ya  Sitalike   ambapo  mtu  mmoja  ambae  nae  jina  lake  limehifadhiwa  kwa  ajiri ya  upelelezi  alikamatwa  akiwa na   jino  moja  la  Simba  akiwa  amerihifadhi  ndani ya  nyumba  yake.
  Mtuhumiwa  alikamatwa baada ya  kufanyika  upekuzi  ndani ya  nyumba yeke  na  ndipo  alipokamatwa akiwa  na  jino  moja  la  samba  akiwa  amehifadhi  ndani ya  nyumba  yake
Kaimu   Kamanda   Damas  Nyanda alisema  watuhumiwa  wote  waliokamatwa  kwenye matukio  hayo   matatu  wanatarajiwa  kufikishwa Mahakamani  wakati wowote  ili  kujibu  tuhuma  zinawazo  wakabili.
Ametowa  wito kwa  wananchi  wanaojihusisha  kufanya  biashara  haramu  za   magendo  kama  vile  uharibifu  wa rasilimali  za Taifa  mfano   vitendo vya ujangili  uwindaji haramu  kuacha  mara  moja  na  badala yake wafanya  shughuli  harali  katika  kujipatia  kipato  chao.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa