Home » » HATARI SANA: WIVU WA MAPENZI WASABABISHA MWANAUME KUMKATA MASIKIO YOTE MAWILI MKE WAKE

HATARI SANA: WIVU WA MAPENZI WASABABISHA MWANAUME KUMKATA MASIKIO YOTE MAWILI MKE WAKE


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Mwanamke mmoja  aliyejulikana  kwa jina la  Agnes Sikazwe (28) Mkazi wa  Kijiji  cha Majimoto  Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi   amekatwa  masiko yake yote mawili  kwa kisu  na mume wake  aliyejulikana kwa jina la Ndomo Mwandu(32) mkazi wa kijiji cha Maji moto  baada ya kumtuhumu kuwa  na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine   
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari  tukio hilo la kukatwa masikio  kwa mwanamke huyo lilitokea hapo Novemba 8 majira ya saa sita na nusu  usiku  nyumbani kwa wanandoa hao wawili waliokuwa wakiishi pamoja
 Alisema kabla ya tukio hilo  wanandoa  hao  wawili walikuwa na ugomvi wa  mara  kwa mara  wa  muda wa  mrefu  ambapo  Ndomo Mwandu  alikuwa akimtuhumu  Agnes  Sikazwekuwa alikuwa  na mahusiano ya kimapenzi na  mwanaume mwingine kijijini  hapo
Kidavashari alieleza siku hiyo ya tukio   wanandoa hao  wawili  walikuwa  wamelala  kitandani   ndipo  mtuhumiwa Ndomo  Mwandu  alipoanza kumtuhumu  Agnes  kuwa  bado anaendelea na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine kijijini hapo
 Alisema   wanandoa hao waliendelea kuzozana  kwa muda mrefu wakiwa kitandani hapo na kisha  Agnes alipitiwa na usingizi na kisha alilala usingizi
 Alieleza  ndipo mtuhumiwa  Ndomo  alipoamka kitandani wakati huo Agnes  akiwa anaendelea  kupiga usingizi  na alichukua  kisu  na kisha  kumkata  masikio yake yote mawili  na kisha kukimbia kusiko  julikana
  Baada ya kufanyiwa  kitendo hicho  Agnes  alipiga mayowe yakuomba msaada kwa majirani ambao walifika kwenye eneo hilo na  kumkuta Agnes akiwa amekatwa masikio yake yote mawili huku mtuhumiwa akiwa ameisha tokomea kusiko julikana
Majirani walimchukua Agnes na kumpeleka kwenye kituo  cha Afya cha Usevya kwa ajiri ya kupatiwa matibabu ambapo amelazwa huku hari yake ikiwa inaendelea vizuri
 Kamanda Kidavashari  alisema  uchuguzi uliofanywa na jeshi la polisi  umebaini kuwa chanzo cha tukio hili ni  wivu wa kimapenzi na  mtuhumiwa   Ndomo Mwandu  bado haja kamatwa  kwani  baada ya kutenda tukio hilo  alikimbia kusiko julikana
 Jeshi la Polisi  linaendelea  na upelelezi  ili kubaini  alikokimbilia  mtuhumiwa  ili waweze kumkamata  na kumfikisha Mahakamani  ili  aweze kujibu  tuhuma  inayomkabili 

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa