Home » » SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA LA TOA MSAADA WA MASHINE ZA KUFYATULIA MATOFARI KWA VIJANA WA MKOA WA KATAVI

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA LA TOA MSAADA WA MASHINE ZA KUFYATULIA MATOFARI KWA VIJANA WA MKOA WA KATAVI

Jiunge na Huduma ya Tone Mobile News Bure kabisa kupitia Whatsapp yako na uwe wa kwanza kupata kile kinachotokea ni Rahisi sana Ingia katika uwanja wa kuandika ujumbe mfupi wa maneno katika Whatsapp yako kisha andika TONE MOBILE NEWS tuma kwenye namba 0756364660 utapokea ujumbe kuwa umeunganishwa.

   Na  walter  Mguluchuma 
Mpanda  Katavi 
Shirika  la  nyumba  la  Taifa   (NHC) limekabidhi  msaada wa mashine  kumi  na mbili  za  kufyatulia  matofali kwa vijana  wa  Halmashauri za  Mkoa  wa  Katavi  zenye  jumla ya  zaidi  ya  shilingi  milioni  tano pamoja  na fedha  tasilimu  shilingi milioni mbili
Msaada huo ulikabidhiwa  hapo jana   kwenye  hafla  iliyofanyika  kwenye  ukumbi  wa  Idara  ya  maji  ulioko  mjini  hapa  ambapo  mgeni  Rasmi  wa  hafla  hiyo  alikuwa   Mkuu wa  Mkoa  wa  Katavi  Dr  Rajabu  Rutengwe
Meneja  wa  Shirila  wa  shirika  la  nyumba  wa Mkoa  wa  Katavi  Nehemia  Msingwa alieleza  kwenye  hafla  hiyo   shirika  hilo  limetowa  msaada  wa  mashine  kumi na  mbili  kwa  vikundi  vinne  vilivyoko  katika  Halmashauri za  Mpanda  mjini , Nsimbo  na  Halmashauri  ya  Wilaya  ya  Mpanda zenye  jumla  ya  thamani  ya  Tsh 5,600,000
Alifafanua kila  Halmashauri  imepatiwa  mashine  nne  kutoka NHC  isipo kuwa  Halmashauri ya  mji wa  Mpanda  ambayo  imepata mashine  sita  ambapo  mashine  mbili zimenunuliwa kwa pesa  tasilimu  na  Halmashauri hiyo  ikiwa  imeanza kutekeleza  agizo la  waziri mkuu   la kuzitaka  kila  Halmashauri  kutenga fungu maalumu  kwa ajili ya kununulia  mashine hizi
 Alisema shirika la  NHC kwa  kushirikiana  na  chuo  cha  ufundi  stsdi  VETA   Mpanda  kimewaandalia  mafunzo  vijana wa vikundi  hivyo  namna  ya kuzitumia  mashine hizo  na ndio  maana   NHC imewapatia  kila  kikundi  kiasi  cha   Tsh   500,000 kwa kila kikundi  kama sehemu ya mtaji  ambao  wanatakiwa wautumie  mara baada ya kumaliza  mafunzo
Msingwa  alieleza  Shirika  la  NHC  limebuni  mpango  huu  mahsusi  kwa ajiri ya kuwasaidia  vijana  mashine za kufyatulia  matofali  na utakuwa ni  endelevu ilikuwasaidia vijana  kujiajiri  wenyewe na kupunguza  tatizo  la  ajira
 Mgeni  Rasmi wa  hafla  hiyo  Dr   Rajabu  Rutengwe  alisema  Serikali  ya  Mkoa wa  Katavi  inatambua  juhudi  zinazofanywa  na NHC  toka  wamefika  katika  Mkoa huu  kumekuwa  na  mabadikliko makubwa  ya kimaendeleo
Alisema ni  vizuri   vikundi hivyo  vilivyopatiwa  msaada huo kuhakikisha vinatumia  hurusa  hiyo   vizuri  na  wajitume  kwenye  elimu wasijione  kama wamechelewa
 Rutengwe  pia  aliwahimiza wazazi wawekeze  watoto wao  kwenye  swala  la  Elimu  hivyo wazazi wahakikishe wanawasomesha watoto wao  ambao hawakwenda Sekondari  wawapeleke kwenye  shule za ufundi
Mkuu wa Mkoa aliziagiza  Halmashauri zote za Mkoa wa  Katavi  zihakikishe  zinatenga maeneo  kwenye   Halmashauri  zao kwa ajiri  ya  ujenzi  wa  nyumba   za  Shirika  la  Nyumba  la Taifa

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa