Home » » ZITO KABWE AKANUSHA KUMUOA MTOTO WA KIKWETE‏

ZITO KABWE AKANUSHA KUMUOA MTOTO WA KIKWETE‏


 Naibu katibu mkuu wa chadema taifa Zitto Kabwe akichangiwa mchango wa mafuta kwa ajili ya gari lake kusafiria kutoka Mpanda kwenda Sikonge mkoani tabora mara alipomaliza kuwahutubia wakazi wa mji wa Mpanda hapo jana kwenye viwanja vya maridadi na ndipo wananchi hao wakajitokeza kwa wingi kumchangia mafuta

 Naibu katibu mkuu wa chadema taifa Zitto Kabwe akiwahutubia wananchi wa Mji wa Mpanda katika viwanja vya maridadi hapo jana ambapo alikanusha uvumi ulionea kuwa amekuwa kimya na amepunguza makali yake bungeni kwa sababu amemuoa mtoto wa Raisi kikwete alikana kumuoa mtoto wa kikwete


Na Walter  Mguluchuma
Mpanda  Katavi yetu Blog
Naibu  katibu  mkuu wa Taifa wa CHADEMA   Zito  Kabwe  amekanusha  uvumi ulioenea  wa kuwa  amemuowa mtoto  wa Rais Kikwete  na ndio maana amepunguza makali yake Bungeni  ya kuuliza maswali  na kuchangia hoja
Zito  alitowa kauli hiyo ya kukanusha uvumi wa  kumuowa mtoto wa Rais Kikwete  hapo jana  juzi wakati  akiwahutubia  maelfu ya wakazi  wa mji wa Mpanda  kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika  kwenye  viwanja vya Maridadi  mjini hapa
Alisema  uko uvumi ambao umeenea hapa nchini  kuwa makali yake yamekupungua  bungeni kutokana  na yeye kumuowa mtoto wa Rais Kikwete wakati sio kweli  yeye hajamuowa mtoto wa Kikwete
Alifafanua kuwa  yeye Bungeni hayuko kwa ajiri ya kupigana ngumi  bali yeye  siku zote toka amekuwa mbunge  amekuwa  akipigania  kutoa hoja zenye nguvu ndani ya Bunge  kama hana hoja za msingi  huwa hakulupuki ovyoovyo
Alieleza ndio maana katika kikao kijacho  cha Bunge  ameisha  wasilisha  maombi ya  mswada binafsi  wa kupendekeza  kufutwa  kwa sheria  ya mwaka 1976 sheria namba 3 ambayo amedai  inavinyima  haki na uhuru vyombo vya habari
Wako viongozi  wamekuwa wakiitumia vibaya sheria hiyo  na hasa pale wanapo kuwa wamekosolewa  au kuandikwa vibaya na magazeti mbona mie Zito  nilikuwa  naandikwa  vibaya na kusingiziwa kuwa  nimejenga nyumba ya gorofa Dodoma wakati hata kiwanja sina Dodoma lakina hata siku moja sija vichukia vyombo vya habari  alisema Zito
Alisema kitendo cha kuyafungia magazeti ya Mtanzania na Mwananchi  ni ukiukwaji wa katiba kwani  kila mwananchi  ana haki ya kupata habari  na kitendo hicho kinapunguza ajira kwa vijana
Alisema leo hii Serikali  inapenda kufanya mambo yake kisiri na ndio maana  hata mishahara yetu sisi wabunge  ambao mmetuchagua  nyinyi wananchi  hamjuwi wakati ni haki yenu  ngoja niwatajie mshara anao pata waziri  na Wabunge
Mshahara  wa Mbunge kwa mwezi anapa kwa mwezi shilingi Tsh 11,200,000 wakati  waziri mkuu anapata mshara wa shilingi milioni 26 kwa mwezi na kila kitu anapata bure  kama ni kosa  kutamka mshahara wa ni kosa basi  namie nichukuliwe hatua  kama magazeti yalivyo fungiwa na kesho nikiwa Wilayani Sikonge  ntataja na Rais anapata mshahara kiasi gani  kwa mwezi
Kuhusu katiba aliomba marekebisho ya katiba  yazingatie zaidi kuwapa mamlaka ya maamuzi wananchi  kuliko  viongozi  kama ilivyo sasa  na alishauri mbunge awe mbunge tuu na asiwe waziri kwani mbunge anapo kuwa waziri  matokeo yake ni wananchi waliomchagua wanakosa uwakilishi bungeni
Alisema  anao mfano hai  kwa  Waziri Mkuu Mizengo Pinda  toka amechaguliwa kuingia Bungeni mwaka 2000 hajawahi  kuuliza  swali hata moja bungeni  kama  kuna mtu  anaushahidi  wa swali lolote ambalo Pinda aliwahi kuuliza  yeye Zito  yuko tayari kumpa shilingi laki mbili mwananchi huyo
Alifafanua kuwa Pinda alichaguliwa kuwa Mbunge kwa mara ya kwanza  na aliteuliwa kuwa naibu wa Tamisemi  hivyo nafasi hiyo ya uwaziri imembana muda wote kuuliza maswali 

Picha  na Katavi yetu Blog

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa