Home » » DC: WAANDISHI WAANDIKE HABARI ZA MAISHA YA WATU WA VIJIJINI‏

DC: WAANDISHI WAANDIKE HABARI ZA MAISHA YA WATU WA VIJIJINI‏


Na Walte Mguluchuma
Mpanda – Katavi
Mkuu wa wilaya ya Nkasi ambae pia ni mlezi wa Klabu ya waandishi wa habari wa Rukwa na Katavi Iddy Kimanta amewataka waandishi wa habari kuandika zaidi habari zinazowahusu watu wenyewe wa vijijini
Ushauri huo aliutoa hapo janqa wakati akizungumza na waandishi wa habari wa mkoa wa Katavi kwenye ukumbi wa Dilux mjini Mpanda.
Kimanta alisema waandishi wa habari wanapoandika habari za vijijini wanachangia kwa kiasi kikubwa kichochea maendeleo ya vijijini ambapo taarifa za kazi mbalimbali za maendeleo zinazokuwa zikifanyika zimekuwa haziandikwi.
Alifafanua kuwa wananchi wa vijijini wamekuwa wakivunjika    sana moyo pale wanapokuwa wamefanya jambo Fulani la maendeleo harafu linakuwa halitolewi na vyombo vya habari
Alieleza zinapoandikwa habari za vijijini kwenye vyombo vya habari vinawafanya hata wananchi wa vijiji vingine waige kilichofanywa na wenzao
Kimanta pia aliwataka waandishi wa habari kuandika habari zinazosaidia kufichua  uozo mbalimbali unaofanywa na taasisi na serikali.
Hivyo pale wanahabari  wanapoona mambo yanakwenda kinyume  ni vizuri waandishi wayaweke wazi  na pale panapokuwa yamefanyika mambo mazuri ya maendeleo yaandikwe pia.
Aidha Kimanta amewaomba viongozi wa serikali wawe tayari pale wanapokuwa wamekosea wanapa kosolewa
Alesema wapo baadhi ya viongozi wamekuwa akiwachukia waandishi wa habari wanapokuwa wametowahabari zenye ukweli halisi unaokuwepo.

1 comments:

Unknown said...

kwailo mkuu umenena kwani uku vijijin tunafanya mambo makubwa na mazuri lakini ayatangazwi

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa