Na Walter Mguluchuma.
Katavi
Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Mkoani Katavi Serikali ya Mkoa huo imeifunga barabara inayounganisha Mkoa wa Katavi na Mkoa wa Tabora fuatia daraja la mto Koga linaloliunganisha mikoa hiyo kujaa maji .
Uamuzi huo wa Swerikali ya Mkoa wa Katavi ulitolewa hapo jana na Mkuu wa Mkoa Meja Generali Raphael Muhuga mbele ya wandishi wa habari muda mfupi baada ya kumaliza kusikiliza kero za wananchi katika uwanja wa michezo wa azimio mjini hapa.
Alisema Serikali ya Mkoa huo imepiga marufuku magari ya aina yoyote ile kupita kwenye daraja hilo kufuatia daraja hilo la mto koga kujaa maji hari ambayo inahatarisha uhai wa watu endapo watapita kwenye daraja hilo .
Alisema agizo hilo sio kwa ajari ya magari ya abiria tuu bali ni kwa ajiri ya magari yote yakiwemo ya mizigo na magari madogo na endapo mtu atakaidi agizo hilo hatua kari zitachukuliwa dhidi yake na kwa lolote lile litakalo kuwa limetokea litakuwa juu yake .
Muhuga alieleza kuwa kuwa barabara hiyo itafunguliwa pindi mvua zitakapo isha na wataalamu wanao simamia barabara watakapo kuwa wameridhika na hari ya daraja hilo baada ya kuwa wamelikagua na kuhakikisha nguzo za daraja zitakapo onekana kuwa zipo salama .
Meneja wa Sumatra wa Mkoa wa Katavi Amani Mwakalebela alisema ofisi yake ipo tayari kutowa vibali kwa ajiri ya mabasi yanayofanya shughuli za kusafirisha abiria kutoka Mpanda kwenda Mkoa wa Tabora kwa kupitia barabara ya Mpanda Uvinza Mkoani Kigoma .
Pia kwa mabasi yanayotoka Mpanda kuelekea Mwanza Sumatra itatowa vibali kwa barabara ya kupitia Mkoa wa Mbeya ili kuweza kufanya abilia waweze kuendelea na safari zao kama kawaida
Daraja la mto Koga ndilo linalounganisha Mkoa wa Katavi na Mkoa wa Tabora na barabara hiyo ndio imekuwa ikitumiwa na magari ya abilia na magari ya mizigo kwa ajiri ya safari za kwenda Mikoa ya Kanda ya ziwa ,Kaskazini na Mikoa ya Kati
MWISHO
0 comments:
Post a Comment