Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu
Waziri wa Madini, Doto Biteko (mwenye kipaza sauti) akizungumza na
wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kwenye machimbo ya Kitunda ya
Wilayani Sikonge, Mkoani Tabora. Biteko alifanya ziara kwenye machimbo
hayo ili kujionea shughuli zinazoendelea sambamba na kuzungumza na
wachimbaji.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Peres Magiri wakiwa kwenye mkutano na wachimbaji wadogo wa machimbo ya dhahabu ya Kitunda yaliyopo Wilayani Sikonge, Mkoani Katavi.
Baadhi
ya Wachimbaji wadogo wa dhahabu kwenye machimbo ya Kitunda wilayani
Sikonge wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo
pichani) alipofika kwenye machimbo hayo ili kujionea shughuli
wanazofanya pamona na kujadiliana nao masuala mbalimbali ikiwemo ulipaji
wa kodi na tozo mbalimbali za Serikali.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Peres Magiri wakiwa kwenye mkutano na wachimbaji wadogo wa machimbo ya dhahabu ya Kitunda yaliyopo Wilayani Sikonge, Mkoani Katavi.
Wachimbaji
wadogo wa dhahabu kwenye machimbo ya Kitunda wilayani Sikonge
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani)
alipofika kwenye machimbo hayo ili kujionea shughuli wanazofanya pamona
na kujadiliana nao masuala mbalimbali ikiwemo ulipaji wa kodi na tozo
mbalimbali za Serikali.
Naibu
Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) akiwasilikiza baadhi ya
Wachimbaji wadogo wa dhahabu kwenye machimbo ya Kitunda wilayani Sikonge
wakiuliza maswali na kuelezea changamoto mbalimbali ziazowakabili kwa
lengo la kuzitafutia ufumbuzi.
Naibu
Waziri wa Madini, Doto Biteko (mwenye kipaza sauti) akizungumza na
wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kwenye machimbo ya Kitunda ya
Wilayani Sikonge, Mkoani Tabora. Biteko alifanya ziara kwenye machimbo
hayo ili kujionea shughuli zinazoendelea sambamba na kuzungumza na
wachimbaji.
Serikali
imesema itawachukulia hatua za kinidhamu watendaji wanaotumia madaraka
yao vibaya kwa kuwanyanyasa wachimbaji wadogo wa madini nchini ili
kujipatia kipato kinyume na taratibu.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko kwenye mkutano na
wachimbaji wadogo wa madini katika machimbo ya Dhahabu ya Kitunda
yaliyopo Wilayani Sikonge, Mkoani Tabora.
Wakielezea
changamoto zinazowakabili, wachimbaji wa machimbo hayo kwa nyakati
tofauti walimueleza Biteko masikitiko yao juu ya unanyasaji
wanayofanyiwa na baadhi ya Maafisa wa Serikali wasiowaaminifu wakiwemo
Askari Polisi na Maafisa Madini.
Wachimbaji
hao walisema kumekuwepo na tabia ya kushinikizwa kutoa rushwa ama
kugawana faida kwa vitisho kuwa watazuiwa kuendelea kufanya shughuli zao
kwenye maeneo husika.
“Kuna
baadhi ya Maafisa Madini na Askari Polisi wamekuwa wakitulazimisha nao
tuwape mgawo wa mawe tunayochimba vinginevyo watafukia maduara yetu,”
alisema Alfred Kulwa mmoja wa wachimbaji kwenye machimbo hayo.
Kufuatia
malalamiko hayo, Naibu Waziri Biteko alitoa onyo kwa watendaji wenye
tabia hiyo kuacha mara moja na alimuagiza Afisa Madini kushirikiana na
Mkuu wa Polisi wa Wilaya husika kuhakikisha wanafuatilia suala hilo na
watakaobainika hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
“OCD,
tendeni haki, hawa wawe salama. Askari atakayebainika ananyanyasa
mchimbaji madini achukuliwe hatua za kinidhamu haraka bila kuchelewa,”
aliagiza Naibu Waziri Biteko.
Biteko
alisema Afisa yeyote anayehitaji kujishughulisha na biashara ya madini
aache kazi ili ajikite katika biashara hiyo na sio kutumia cheo chake
kuwanyanyasa wachimbaji.
Aliongeza
kuwa hairuhusiwi Mtumishi wa Umma kutumia cheo kujinufaisha. “Marufuku
watendaji wa Serikali ama wamiliki wa leseni za uchimbaji madini kutumia
madaraka yao vibaya. Kama unataka ingia uchimbe mwenyewe. Serikali hii
ya Awamu ya Tano inatutaka tuondoe manyanyaso,” alisema Biteko.
Biteko
alisema mchimbaji atakayenyanyaswa atoe taarifa Polisi na pia
amfahamishe kwa njia ya simu kuhusiana na manyanyaso hayo ambapo alitaja
namba zake za simu ili kukitokea hali ya sintofahamu wasisite
kumfahamisha.
Hata
hivyo, Biteko aliwataka wachimbaji hao kuacha kuwasilisha taarifa za
uwongo ikiwemo kusingiziana na mara zote wasimamie haki ili kuepusha
migogoro baina yao na Serikali.
0 comments:
Post a Comment