Na Walter Mguluchuma.
Katavi
Waratibu wa TASAF wa mpango katika ngazi ya Mkoa ,Halmashauri ,Maafisa ufuatiliaji wa mpango na Wandishi wa Habari katika Mkoa wa Katavi wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuhakikisha kuwa wanatangaza na kuelimisha wananchi kuhusu malengo ya mpango wa TASAF .
Wito huo ulitolewa hapo jana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali Raphael Muhuga katika hotuba yake ilisomwa kwa niaba yake na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uelewa Wandishi wa Habari wa Mkoa wa Katavi kuhusu mpango wa kunusuru Kaya maskini yaliofanyika katika ukumbi wa Kichangani Mjini hapa .
Alisema mafunzo hayo yatawapa furusa Wandishi wa Habari ya kupata taarifa za maendeleo ya utekelezaji wa Mpango katika Mkoa wa Katavi na kufahamu dhana mbalimbali za mpango wa Tasaf katika Mkoa huo .
Aliwasisitiza Waratibu wa mpango wa Tasaf na wahasibu wa Halmashauri kuhakikisha kuwa nyaraka zote muhimu za mpango zikiwemo nyaraka za malipo zilizopo Halmashauri nakala zake zinakuwepo pia katika Vijiji na Mtaa inayotekeleza mpango huo.
Pia alizitaka kila Halmashauri ijiwekee mkakati wa kuwahamasisha wanufaika wa mpango wa Tasaf wanajiunga na mfuko wa Afya ya jamii.
Aliwaomba Wandishi wa Habari washirikiane kwa pamoja kutangaza utekelezaji wa Mpango wa Tasaf katika Mkoa huo kwani mambo mengi mazuri yanafanyika lakini hayatumiki kuwasaidia watu wengine wajifunze kutokana na mpango wa Tasaf.
Hivyo ni matumaini yake kuwa waratibu wa mpango katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri watawatumia wandishi wa Habari katika ziara zao watakazo fanya ili kuweza kuutangaza mpango huu.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Tasaf Zuhura Mdungi alisema Tasaf awamu ya tatu inatekeleza mpango wa kunusuru kaya maskini ambao unawezesha kaya zilizoandikishwa kupata ruzuku ili kumudu mahitaji ya msingi kama elimu ,afya na lishe na kuwekeza katika miradi ya ujasilimali .
Alifafanua kuwa madhumuni ya mpango ni kuziwezesha kaya maskini kuwa na uhakika wa chakula ,kujenga rasilimali , watoto na kutoa fursa kwa kaya kuongeza kipato .
Mraribu wa Tasaf wa Mkoa wa Katavi Ignas Kikwala alieleza kuwa mafunzo hayo yatawajengea uwezo wandishi wa uwelewa wa pamoja wa masuala muhimu kuhusu mpango wa kunusuru Kaya maskini na kupeana taarifa za utekelezaji kwa wandishi wa habari ili waweze kupata wigo mpana wa kutangaza utekelezaji wa Mpango wa Tasaf katika Mkoa huu.
Alisema Mkoa wa Katavi una vijiji 177 ila vijiji vinavyotekeleza mpango wa Tasaf awamu ya tatu vipo 80 kwa mwaka 2014 Mkoa ulikuwa na kaya 8,537 zilinufaika na mpango huu kwa sasa zimebaki kaya 7,668 .
Kaya hizo zimepungua kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kwa kaya ,kufariki kwa wanufaika wa mpango ,,baadhi ya kaya kupata nafasi za uongozi katika Serikali za vijiji Mtaa na wengine kuondolewa kwa kukosa sifa.
0 comments:
Post a Comment