Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Wakala wa Barabara TANROAD Mkoa wa Katavi umeomba kutengewa jumla ya Tshs Bilioni 27.534 kwa ajiri ya Bajeti ya Mwaka wa fedha wa 2018/ 2019 kwa ajiri ya kufanya matengenezo ya barabara zenye urefu urefu km 1,203 na kwa ajiri ya kulipia fidia ,kufanya ukarabati wa barabara ,kufanya usanifu wa kina na kujenga madaraja .
Mapendekezo hayo ya bajeti yalisomwa hapo jana na Kaimu Meneja wa Tanroods wa Mkoa wa Katavi Eng Martin Mwakabende wakati aliokuwa akisoma taarifa ya utekelezaji wa kazi za matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2017/ 2018 na alipokuwa akiwasilisha mapendekezo ya bajeti ya fehda mwaka wa fedha 2018/ 2019 kwenye kikao cha bodi ya barabara cha Mkoa wa Katavi kilichofanyika katika ukumbi wa maji mjini hapa .
Aiisema Wakala wa barabara Mkoa wa Katavi unahudumia mtandao wa barabara wenye jumla ya kilometa 1,1o1.46 huku barabara kuu zikiwa ni kilomeeta 474.30 barabara za Mkoa ni kilometa 627.16 kilometa 58.41 ni za kiwango cha lami na barabara za changalawe ni kilometa 1,043.
Alisema katika mwaka wa fedha wa 2017/2018 Mkoa umetengewa Bajeti ya Tshs Bilioni 14.392 kwa ajiri ya kufanya matengezo na ukarabati wa barabara ambapo mfuko wa barabara ni kiasi cha Tshs Bilioni 12,434 na fedha za maendeleo ni Tshs Bilioni 1.968 na hadi sasa wamepokea fedha kwa ajiri ya matengenezo ya barabara kutoka katika mfuko wa barabara kiasi cha Tshs Bilioni 6.062 kiasi hicho ambacho ni sawa na asilimia 48.75 ya fedha zilizoidhinishwa.
Mwakabende alieleza kuwa Wakala wa Barabara unaendelea kuthibiti magari mazito kwa kuyapima na gari ambalo likibainika limezidisha uzito hutozwa gharama ya uharibifu kwa mujibu wa sheria ya usalama barabarani ya mwaka 1973 lengo ikiwa ni kutunza usalama na kudhibiti uzito wa magari barabarani .
Nae Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga aliwataka Wakala wa Barabara wa Mkoa wa huu kuhakikisha wanaendelea kufungua barabara mpya ambazo zinaweza kuwafikia mwananchi ili waweze kusafirisha mazao yao na kukuza uchumi .
Alisema barabara zikiwepo kwenye maeneo wanayoishi wananchi zinasaidia sana hasa kwenye Mkoa huu unaopakana na Nchi za jirani Kongo DRC, na Burundi katika swala zima la usalama kwenye maeneo ya mipakani .
MBunge wa Jimbo la Mpanda Vijiji Moshi akichangia bajeti hiyo alisema zipo barabara za zamani zilizokuwa zikiwaunganisha watu wa Mkoa huo na Mikoa ya Rukwa na Kigoma pamoja na wanao ishi pembezoni mwa ziwa Tanganyika .
Alizitaja baadhi ya barabara ambazo zinatakiwa kuunganishwa kuwa ni Mlibasi kwenda Ziwa Tanganyika itakayo unganisha Mishamo na Mkoa wa Kigoma na Karema Kabwe ambayo itawasaidia sana wananchi wa Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi na wale wa Wilaya ya Nkasi Mkoa wa Rukwa .
MWISHO
0 comments:
Post a Comment