MASUNJU MGELU AKIWA AMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA MANISPAA YA
MPANDA BAADA YA KUPIGWA RISASI YA MGUU WAKE WA KUSHOTO NA MAJAMBAZI
WATATU WALIOVAMIMIA MACHIMBO YA DHAHABUHUKO ISUMAMILOMO KWA KUTUMIA
BUNDUKI YA KIVITA AINA YA AK 47 AMBAPO KATIKA TUKIO HILO MCHIMBAJI
MMOJA ALIUAWA KWA KUPINGWA RISASI TUMBONI NA WATATU KUJERUHIWA
AMBAPO MAJAMBAZI HAO WALIPORA DHAHABU GRAMU 650,MASHINE MBILI ZA
KUTAFUTIA DHAHABU NA FEDHA TASILIMU TSHS 1,500,000
PICHA NA WALTER MGULUCHUMA-KATAVI YETU
PICHA NA WALTER MGULUCHUMA-KATAVI YETU
Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamevamia machimbo ya madini ya dhahabu ya Ifumile Kijiji cha Isumamilomo Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda na kuuwa mchimbaji mmoja kwa kumpiga risasi tumboni kwa kutumia bunduki ya kivita na kujeruhi wengine watatu katika sehemu zao mbalimbali za mwili na kisha kupora dhahabu ya zaidi ya Gramu 600,fedha tasilimu Tshs 1,500,000 na mashine mbili za kutafutia dhahabu .
Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda aliwaambia wandishi wa Habari kuwa tukio hilo la ujambazi lilitokea hapo juzi majira ya saa saa mbili usiku katika machimbo hayo ya madini ya dhahabu .
Alisema siku hiyo ya tukio majambazi hao waliokuwa watatu walifika katika machimbo ya dhahabu ya Ifumile yaliko katika Kijiji cha Isumamilomo huku wakiwa wamejifunika sura zao usono KININJA na kuwashambulia kwa risasi za moto wachimbaji na wanunuzi wa dhahabu kwenye machimbo hayo .
Katika shambulio hilo waliweza kuwajeruhi vibaya kwa risasi wachimbaji wanne katika sehemu zao mbalimbali za mili yao huku baadhi ya wachimbaji walikuwa kwenye eneo hilo waliweza kusalimika baada ya kuwa wamekimbilia kwenye vichaka .
Kamanda Nyanda aliwataja majeruhi walijeruhiwa kwa kupigwa risasi kuwa ni Sita Kalyalya 34 Mkazi wa Bariadi Shiyanga ambae alipingwa risasi ya tumboni na mkononi aliyefariki Dunia muda mfupi baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Manispaa ya Mpanda wakati akiwa anapatiwa matibabu .
Wengine waliojeruhiwa ni Joseph Panya 34 ambae amereruhiwa vibaya kwenye bega la kushoto na mguu wa kulia Mrisho Rashid 21 aliyejeruhiwa mguuni na mkono wake wa kulia na Masunju Mgulu 28 aliyejeruhiwa mguu na mkono wake wa kushoto .
Kamanda Nyanda alisema majambazi hao watatu hao baada ya kuwajeruhi wachimbaji hao waliweza kupora fedha tasilimu Tshs 1,500,000 Gramu 650 za madini ya dhahabu na masine mbili za kutafutia madini na kicha walitokomea kusiko julikana.
Mara baada ya tukio hilo polisi walifika kwenye eneo hilo hata hivyo waliweza kuokota Risas 24 za moto na maganda saba ya risasi zilizotumika za bunduki ya kivita iliyotumika kwenye tukio hilo aina ya AK 47.
Alisema Jeshi la polisi Mkoa wa Katavi bado linaendelea kuwasaka majambazi waliohusika kwenye tukio hilo na wametowa wito kwa wananchi kutowa ushirikiano kwa jeshi hilo kwa kuwapatia taarifa zitakazowawezesha kuwatia nguvuni watuhumiwa watukio hilo .
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Manispaa ya Mpanda Dr Masanja alisema marehemu Sita Kalyalya alifariki muda mfupi baada ya kuwa ametolewa kwenye chumba cha upasuaji ambako alikuwa akipatiwa matibabu ya kuunganishiwa utumbo wake mkubwa ambao ulikuwa umekatika kutokana na kupigwa risasi tumboni .
Alisema majeruhi Joseph Panya na Mrisho Rashid hao ambao walikuwa wamelazwa katika wodi namba moja wamepewa rufaa na wamesafirishwa kwenda katika hospitali ya Rufaa ya Muhimbili kwa ajiri ya matibabu zaidi baada ya hari zao kuwa mbaya sana ambapo majeruhi Masunju Mgelu yeye amebaki kwenye hospitali hiyo huku hari yake ikiwa inaendelea vizuri.
0 comments:
Post a Comment