Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Mwanafunzi wa darasa la sita Shule ya Msingi Vikonge Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi mwenye umri wa miaka 14 ameuawa kikatili baada ya kubakwa na kuchomwa kisu ubavuni na kisha kunyofolewa sehemu za siri wakati akiwa anakwenda shuleni na mdogo wake wa liokuwa wakisoma shule moja .
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Damas Nyanda alisema tukio la kuuawa kwa mwanafunzi huyo wa kike lilitokea hapo jana majira ya saa moja na nusu Asubuhi umbali wa kilometa moja na nusu kutoka katika shule ya Msingi Vikonge.
Alisema siku hiyo ya tukio marehemu huyo alitoka nyumbani kwao kwa lengo la kwenda shuleni kama ambavyo ilivyokuwa kawaida yake huku akiwa na mdogo wake wa kiume mwenye umri wa miaka 11 mwanafunzi wa darasa la nne shule ya Msingi vikonge ambae jina lake limehifadhiwa .
Wakati wakiwa njiani alitokea mwendesha pikipiki moja ambae walikuwa hawamfahamu na kusimamisha pikipikiyake na kisha aliwaambia kuwa awape msaada wa usafiri wa kuwafikisha shuleni kwao .
Kamanda Nyanda alieleza baada ya kuambiwa hivyo wanafunzi hao walikubali kupewa msaada wa pikipiki hata hivyo mara baada ya marehemu kuwa amepanda pikipiki hiyo mwendesha boda boda huyo alimzuia mdogo wa marehemu asipande kwenye pikipiki hiyo na kisha aliiondoa huku akiwa na marehemu na kumwacha kaka yake .
Hari hiyo ilimfanya kaka yake aamue kuifuata pikipiki hiyo kwa nyuma na ndipo wakati akiwa njiani aliona pikipiki kama ile iliyokuwa imembeba dada yake ikiwa kwenye kichaka pembeni ya barabara hata hivyo aliendelea na safari yake ya kwenda shuleni .
Kaka huyo wa marehemu kutokana na kuwa na umri mdogo baada ya kufika shuleni hakuweza kumtafuta dada yake na badala yake aliingia darasani na kuendelea na masomo kama kawaida na baada ya muda wa masomo ilipofikia majira ya saa nane na nusu alianza safari ya kurejea nyumbani pasipo kumtafuta dada yake.
Kamanda Nyanda alieleza baada ya kuwa amefika nyumbani kwao wazazi wake walishituka kumwona akiwa peke yake ndipo walipomuuliza aliko mwacha dada yake na aliwaeleza mazingira yote ya jinsi alivyo achana na dada yake wakati walipokuwa njiani na jindi alivyoiona pikipiki iliyombeba dada yake ilivyokuwa kwenye kichaka .
Wazazi wa marehemu baada ya kupata maelezo hayo walipatwa na mashaka hivyo walimtaka mdogo wa marehemu awapeleke kwenye eneo aliloona pikipiki ikiwa kwenye kichaka .
Alisema Wazazi wa marehemu waliokuwa wameongozana na majirani zao baada ya kufika kwenye eneo hilo walishitushwa kuona majani yakiwa yakiwa yamelala na ndipo walipoenda mbele kidogo waliweza kuukuta mwili wa marehemu ukiwa amechomwa kifu sehemu ya ubabu wake wa kulia na sehemu za siri zikiwa zimenyoforewa .
Kamanda wa polisi Damas Nyanda alisema jeshi la polisi Mkoa wa Katavi linaendelea na msako wa kumtafuta mtu au watu waliohusika na mauwaji hayo ya kikatili hadi sasa hakuna mtu wla watu waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo .
Kaimu mwalimu Mkuu wa Shule ya Vikonge Mwalimu Gadinendi Kaseka alisema mpaka walipomaliza masomo ya siku hiyo hawakuwa na taarifa juu ya kifo cha mwanafunzi huyo ila walipata taarifa hiyo siku hiyo hiyo majira ya saa kumi na mbili jioni baada ya mwili wa marehemu kuwa umepatikana .
0 comments:
Post a Comment