Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Serikali inatarajia kuiunganisha Mikoa ya Rukwa ,Katavi na Kigoma kwene mradi wa umeme wa Grid ya Taifa ifikapo mwaka 2021 ujenzi wa mradi huo utakuwa umekamilika ilikuifanya Mikoa hiyo kuwa na umeme wa uhakika .
Kauli hiyo ya Serikali ilitolewa hapo jana na Waziri wa Nishati Medadi Kalemani wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Katavi kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi wakati wa ziara yake ya siku mbili ya kukagua miradi ya kufua umeme ya Kampuni na Mlele .
Alisema taratibu za kuanza kwa ujenzi wa mradi huo zipo zinaendelea na zipo katika hatua ya mwisho na kwa kuwa mradi huo ni waumbali mrefu wataweka vituo vya kupozea umeme miuongoni mwa vituo hivyo kimoja kitajengwa Wilayani Mpanda .
Waziri Kalemani alieleza mradi huo utaunganishwa kuanzia Tunduma Sumbawanga , Sumbawanga Mpanda na Mpanda Kigoma yakalanzi na unatarajiwa kukamilika kabisa ifika 2021.
Alisema mradi huo ni lazima utakamilika kwa muda huo uliopangwa na utaondoa kabisa tatizo la Mikoa hiyo kuwa na umeme mdogo na utafanya viwanda vifanya kazi mpaka kwenye maeneo ya vijijini hivyo alitowa wito kwa wawekezaji kuwekeza kwenye Mikoa hiyo .
Alifafanua kuwa lengo la Serikali ni kupeleka umeme kwenye vijiji vyote na taasisi zote na katika Mikoa hiyo ifikapo 2021 hakuna kijiji chochote ambacho kitakuwa hakina umeme wa Rea .
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja generali Mstaafu Raphae Muhuga alisema Mkoa huo katika kuboresha na kuvutia wawekezaji kuwekeza na kuanzisha viwanda na katika kutekeleza sera za serikali ya awamu ya tano ya uchumi wa viwanda , Mkoa umetenga hekta 46,608 kwa ajiri ya uwekezaji na viwanda .
Pamoja na jitihada hizo za Mkoa kutenga maeneo hayo makubwa lakini Mkoa hauja unganishwa na Grid ya Taifa na nishati na umeme kutotoshereza hari hiyo inarudisha nyuma jitihada za Mkoaa .
Muhuga alisema Mkoa wa Katavi unapata umeme kwa kutumia vyanzo viwili ambavyo ni Jenereta tatu na Grid ya kutoka Zambia kupitia Mkoa wa Rukwa kwa baadhi ya maeneo ya Halmashauri ya Mpimbwe Wilayani Mlele.
Nae Mwandisi wa Mradi wa kufua umeme Stephen Manda alisema miradi mingi ya Tanesco imekuwa ikikabiliwa na baadhi ya changamoto mbalimbali .
Alitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni tabia ya watu kulima chini ya nguzo za umeme hari ambayo imekuwa ikisababisha uharifu wa nguzo za umeme na shirika kuingia kwenye gharama za matengenezo yasiyo na sababu .
0 comments:
Post a Comment