Home » » JELA MIAKA 30 KWA KOSA LA KUKAMATWA NA MENO YA TEMBO YA ZAIDI YA MILIONI 90 NA FAINI YA MILIONI 99.

JELA MIAKA 30 KWA KOSA LA KUKAMATWA NA MENO YA TEMBO YA ZAIDI YA MILIONI 90 NA FAINI YA MILIONI 99.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



 Na  Walter  Mguluchuma .
        Katavi .
Mahakama ya  Wilaya ya  Mpanda Mkoani  Katavi imemuhukumu  aliyekuwa   Raia wa  Nchi ya  Burundi   alipata urai wa Tanzania  miaka ya   hivi  karibuni   Jackison  Eijuel 52   Mkazi wa   Makazi ya Wambizi ya Katumba kutumikia jela kifungo cha  miaka 30    na kulipa faini ya    TSHS  mIlioni 99 baada ya kupatikana na  hatia ya kukamatwa na  meno ya  Tembo manne na  vipande   vinne sawa na Tembo watatu  yenye  thamani ya zaidi ya  TSHS 90.
  Hukumu  hiyo  ilitolewa  hapo  jana  na  Hakimu   Mkazi   Mfawidhi wa  Mahakma ya  Wilya ya  Mpanda   Chiganga  Ntengwa  baada ya  kuridhika  na  ushahidi uliotolewa   Mahakamani   hapo  na  upande wa mashitaka  ambapo mshitakiwa  hakuwa na shahidi yoyote kwa upande wake .
   Akisoma hukumu  hiyo   Hakimu   Chiganga  alisema  Mahakamani  hapo  kwamba  mtuhumiwa  amethibitika  kutenda kosa  hilo    kinyume  na  kifungu  cha   sheria  namba  235  cha   mwenendo  wa  mashitaka .
 Alisema  baada ya  kusikiliza  utetezi wa mshitakiwa       Mahakama   imethibisha   pasipo  shaka yoyote  kuwa  mshitakiwa  amepatikana  na  hatia ya  kukamatwa   akiwa  na  meno ya  tembo .
Awali   mwendesha  mashitaka  Mwanasheria wa  Serikali     Fraviani   Shiyo   alidai   Mahakamani  hapo  kuwa   mshitakiwa   Jackisoni    Elijuel alitenda  kosa  hilo  hapo    oktoba  25  mwaka huu  majira ya saa  mbili na  nusu  usiku  huko  katika   Kijiji  cha Urwila    Tarafa ya  Nsimbo  Wilaya ya  Mpanda .
  Aliiambia   Mahakama   kuwa  mshitakiwa    alikamatwa  na   askari  maalumu wa  kuzuia   ujangili wa  pori   la   Ugala  baada ya  kuwa  wamepata  taarifa       za  mshitakiwa     kujihusisha  na  biashara  haramu ya kuuza    meno ya  tembo .
  Fraviani   alieleza  baada ya  askari hao  kuwa  wamepata  taarifa  hizo  ndipo  walipoandaa  mtego na  waliweza     kumkamata   mshitakiwa   akiwa  na   meno  ya   Tembo manne   mazima  na  vipande   vinne vyenye  uzito wa  kiligramu  27  yenye  thamani ya  Tshs milioni 99  ambayo ni  sawa  na  Tembo  watatu wazima
Mshitakiwa  katika  utetezi  wake  aliomba  Mahakama  imwachie  huru kwa  kile  alichodai   kuwa   meno   ya  Tembo  ambayo  alikamatwa  nayo  hayakuwa yak wake  bali yalikuwa  ni  ya  mtu  mmoja   aliyemtaja kwa  majina ya    Hussen  Samora    ndie   aliyekuwa  amemtuma kuyabeba kwa kutumia  pikipiki  yake   mshitakiwa .
 Baada ya  utetezi huo  kabla ya  Hakimu   kusoma  hukumu Wakiri wa  Serikali     Fravian  aliitaka   Mahakama  itowe   adhabu kali kwa   mshitakiwa   il  iwe   fundisho kwa watu  wengine  kwani   vitendo vya  ujangili   zimezidi  kushamili  Mkoani  Katavi .
  Baada ya  kusikiliza  utetezi  wa  mshitakiwa   alitaka  mshitakiwa  ataje    Mahakamani  hapo  namba  za  pikipiki  ambayo        alidai ni  mali yake  aliyoitumia   kubebea  men ohayo ya   Tembo   na  amekuwa  akiiendesha  kwa kipindi  cha miaka  miwili  hata  hivyo mshitakiwa  alishindwa kuzitaja   namba  hizo za pikipiki   aliyodai ni ya  kwake .
 Akisoma  hukumu  hiyo  Hakimu   Mkazi  Chiganga   Ntengwa   alisema   alisema    mshitakiwa  Jackisoni  amepatikana  na   hatia   kinyume  na  kifungu  cha   sheria   namba  235 ya   mwenendo wa  mashitaka   hivyo   Mahakama  imemuhukumu mshitakiwa kutumikia kifungo cha miaka 30  jela na kulipa  faini ya Tshs milioni 99,000,000.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa