Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imemuhukumu aliyekuwa Raia wa Nchi ya Burundi alipata urai wa Tanzania miaka ya hivi karibuni Jackison Eijuel 52 Mkazi wa Makazi ya Wambizi ya Katumba kutumikia jela kifungo cha miaka 30 na kulipa faini ya TSHS mIlioni 99 baada ya kupatikana na hatia ya kukamatwa na meno ya Tembo manne na vipande vinne sawa na Tembo watatu yenye thamani ya zaidi ya TSHS 90.
Hukumu hiyo ilitolewa hapo jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakma ya Wilya ya Mpanda Chiganga Ntengwa baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo na upande wa mashitaka ambapo mshitakiwa hakuwa na shahidi yoyote kwa upande wake .
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Chiganga alisema Mahakamani hapo kwamba mtuhumiwa amethibitika kutenda kosa hilo kinyume na kifungu cha sheria namba 235 cha mwenendo wa mashitaka .
Alisema baada ya kusikiliza utetezi wa mshitakiwa Mahakama imethibisha pasipo shaka yoyote kuwa mshitakiwa amepatikana na hatia ya kukamatwa akiwa na meno ya tembo .
Awali mwendesha mashitaka Mwanasheria wa Serikali Fraviani Shiyo alidai Mahakamani hapo kuwa mshitakiwa Jackisoni Elijuel alitenda kosa hilo hapo oktoba 25 mwaka huu majira ya saa mbili na nusu usiku huko katika Kijiji cha Urwila Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda .
Aliiambia Mahakama kuwa mshitakiwa alikamatwa na askari maalumu wa kuzuia ujangili wa pori la Ugala baada ya kuwa wamepata taarifa za mshitakiwa kujihusisha na biashara haramu ya kuuza meno ya tembo .
Fraviani alieleza baada ya askari hao kuwa wamepata taarifa hizo ndipo walipoandaa mtego na waliweza kumkamata mshitakiwa akiwa na meno ya Tembo manne mazima na vipande vinne vyenye uzito wa kiligramu 27 yenye thamani ya Tshs milioni 99 ambayo ni sawa na Tembo watatu wazima
Mshitakiwa katika utetezi wake aliomba Mahakama imwachie huru kwa kile alichodai kuwa meno ya Tembo ambayo alikamatwa nayo hayakuwa yak wake bali yalikuwa ni ya mtu mmoja aliyemtaja kwa majina ya Hussen Samora ndie aliyekuwa amemtuma kuyabeba kwa kutumia pikipiki yake mshitakiwa .
Baada ya utetezi huo kabla ya Hakimu kusoma hukumu Wakiri wa Serikali Fravian aliitaka Mahakama itowe adhabu kali kwa mshitakiwa il iwe fundisho kwa watu wengine kwani vitendo vya ujangili zimezidi kushamili Mkoani Katavi .
Baada ya kusikiliza utetezi wa mshitakiwa alitaka mshitakiwa ataje Mahakamani hapo namba za pikipiki ambayo alidai ni mali yake aliyoitumia kubebea men ohayo ya Tembo na amekuwa akiiendesha kwa kipindi cha miaka miwili hata hivyo mshitakiwa alishindwa kuzitaja namba hizo za pikipiki aliyodai ni ya kwake .
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Chiganga Ntengwa alisema alisema mshitakiwa Jackisoni amepatikana na hatia kinyume na kifungu cha sheria namba 235 ya mwenendo wa mashitaka hivyo Mahakama imemuhukumu mshitakiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela na kulipa faini ya Tshs milioni 99,000,000.
No comments:
Post a Comment