Mpanda
OFISA Ardhi Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi , Hisim Zuberi Muyiga (49) ameuawa kikatili kwa kunyongwa na watu wasijulikana na kuutelekeza mwili wake shambani .
A
Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa , George Kyando amethibitisha kuawa kwa
Ofisahuyo wa Ardhi kwamba mwili wake uligunduliwa na wananchi kwenye shamba la mifugo la Kanisa la Efathaa ambalo lipo katika kijiji cha Malonje , Manispaa ya Sumbawanga .
“Baada ya mwili huo kugundulika shambani humo na wananchi ambao waliutaarifu uongozi wa kijiji hicho na shamba hilo ambao walitoa taarifa Polisi ….
Askari Polisi walipofika kwenye eneo hilo la tukio waliukuta mwili huo lakin mazingira yanaonesha kuwa aliuawa sehemu nyingine tofauti na hapo kisha ukatupwa shambani humo kwa sasa hakukuwa na purukushani zinazoashiria mtu aliuawa hapo “ alieleza Kamanda .
Aliongeza kuwa baada ya kupekuliwa askari polisi waliweza kukuta leseni yake ya udereva ikiwa mfukoni mwa suruali aliyokuwa ameivaa ambapo waliingiza kadi hiyo ya leseni kwenye mtandano na kubaini kuwa alikuwa ni Ofisa Ardhi , Manispaa ya Mpanda.
“Tuliwasiliana na ndugu zake ambao walikuwa Jijini Dar Es Salaam ambao walitueleza kuwa marehemu aliwaeleza kuwa alikuwa ana safari kwenda mjini Sumbawanga siku moja kabla ya Sikukuu ya Krismasi akiwa na fedha taslimu ya zaidi ya Sh milioni 20/- ….. “ alieleza Kyando .
Aliongeza kuwa baada ya kuwasilina na ndugu za marehemu walioko Jijini Dar Es Salaam mmoja wao aliwaeleza Polisi kuwa marehemu aliwafahamisha ndugu zake kuwa alikuwa amesafiri na gari lake hadi mjini Sumbawanga akiendesha mwenyewe ..
“Sisi Polisi tulianza upelelezi
wetu na kuanza msako wa kulitafuta gari la marehemu ambapo tulilikuta
likiwa limeegeshwa kwenye nyumba ya kulala wageni ya Ligula iliyopo mjini Sumbawanga “ alieleza .
Alitaja gari hilo la marehemu kuwa aina ya Nissan Navara yenye namba za usajiri T 976 CEJ likiwa limeegeshwa kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni .
“Tulipowahoji wahudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni walikiri
kuwa gari hilo ni mali ya marehemu ambaye walimtaja kwa majina yake
wakisisitiza kuwa ni mteja cwao wa kudumu kuwa mara kdhaa amekuwa
akifikia na kulala hapo …..
Walidai kuwa siku hiyo alipofika hapo alichukua chumba cha kulala na kukilipia kisha akaingia ndani baada ya muda mfupi alitoka akiwa amebeba begi jekundu lakini hakurudi tena hadi tulipofika hapo na kuwaeleza yaliyomsibu ambapo walibaki wakiwa wamepigwa na butwaa wakiwa hawamini waliyoyasikia " .alieleza
Kamanda Kyando alieleza kuwa kwa sasa Polisi inafanya uchunguzi wa awali wa kuipekua simu ya marehemu ya mkononi kitaalamu ili kumbaini mtu wa mwisho aliyewasiliana nae na eneo alilokuwepo wakati akiwasiliana na marehemu ili sheria iweze kuchukua mkondo wake .
No comments:
Post a Comment