Na Walter Mguluchuma.
Mlele
WAKULIMA wawili wa kijii cha Majimoto , John Kalikwenda (50) na Kapufi Mdagula (40) wamehukumiwa kila mmoja wao kutumikia kifungo cha miaka saba jela baada ya kukiri kupatikana na silaha aina ya gobole , risasi zake 19 na vilipuzi nyenye uzito wa kilo 100 .
Akitoa hukumu hiyo jana , Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi , Teotimus Swai katika kosa
la kwanza la kukutwa na silaha kila mmoja alihukumiwa kifungo cha miaka
mitano jela huku kosa la pili la kukutwa na risasi 19 kila mmoja alihukumiwa kutoa faini ya Sh 500,00/-.
Hakimu Swai katika kosa la tatu la kukutwa na vilipuzi kila mmoja wa washtakiwa hao alihukumiwa kwenda jela miaka saba au kkulipa faini ya Sh milioni moja .
“ Kwa kuwa adhabu hizo zinaenda kwa pamoja kila mshtakiwa atatumikia kifunga jela miaka saba au kulipa faini ya Sh milioni moja …. Mahakama hii imetoa adhabu kali ili iwefundisho kwa wengine wenye tabia kama zao “ alieleza.
Hata hivyo washtakiwa hao wameanza kutumikia adhabu hiyo baada ya kushindwa kulipa faini hiyo .
Awali
Mwendesha Mashtaka , Mkaguzi wa Polisi , Bahati Hongoli alidai
mahakamni hapo kuwa washtakiwa hao wawili walitenda kosa hilo Aprili 27,
mwaka huu saa nane mchana ambapo walikamatwa wakiwa ndaji ya Hifadhi ya
Wanyamapori ya Rukwa – Lwafi iliyoko wilayani Mlele .
Ilielezwa mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Mei ,3,2017.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment