MIMBA za utotoni bado ni tishio kubwa katika
Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi ambako wasichana 624 walio na umri
wa chini ya miaka 18 wamejifungua katika Vituo vya Afya vilivyopo
katika manispaa hiyo .
Hayo
yalisemwa hapo jana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali
mstaafu Raphael Muhuga, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya siku
16 za kupinga ukatili wa kijinsia zilizofanyika kimkoa
katika viwanja vya Saba Saba kijijini Kabungu Wilayani Tanganyika .
Muhuga
alisema taarifa kutoka katika vituo vya afya vya Manispaa ya
Mpanda ya kipindi cha mwaka jana wa 2016 inaonyesha kuwa wasichana
624 wenye umri wa chini ya miaka 18 walijifungua katika vituo vya
Afya vilivyopo katika manispaa hiyo kwamba kiwango hicho ni
kikubwa na tishio ..
Alisma
hari hiyo ya mimba za utotoni imekuwa ikifanya watu wanao
tembea barabarani au kwenye masoko ya Manispaa ya Mpanda
kukutana na watoto ambao wamezaa wakiwa na umri mdogo huku mgongoni
wakiwa wamebeba watoto wenzao.
Alifafanua alisema utafiti
wa afya ya uzazi na mtoto na viashiria vya maralia wa mwaka
2015 na 2016 uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS kwa
kushirikiana na Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto kwa Tanzania umeonyesha mkoa wa Katavi ujaongoza
kitaifa kwa mimba za utotoni.
Aliongeza
kuwa utafiti huo umeonyesha kuwa kitaifa asilimia 27 ya
wasichana wa miaka 15 hadi 19 wameishaanza uzazi asilimia
21 walikuwa wameisha zaa mtoto hai angalau mmoja huku katika mkoa
wa Katavi asilimia 45 ya wasichana wa miaka 15 hadi 19
wameisha anza uzazi ,ambapo asilimia 33.3 wakiwa wameshazaa mtoto
hai angalau mmoja. .
Kuhusu
unyanyasaji wa kijinsia Muhuga lisema kuwa i jumla ya kesi 1,178
zililipotiwa katika vituo vya kutolea huduma za afya mkoani
humo na maofisa ustawi wa jamii katika mwaka 2016.
Muhuga
alisema kati ya kesi hizo 401 zilihusu ukatili wa kimwili , kesi
66 zilihusu ukatili wa kingono ,kesi 264 zilihusu ukatili wa
kisaikolojia na kesi 447 zilihusu kutelekezwa watoto na familia zao
kwamba wa ukatili wa kimwili au ngono ulifanywa na wanaume .
Kwa upande wake Mkuu
wa Wilaya ya Mpanda Liliani Matinga aliwataka wanawake
ambao wanatabia ya kupiga waume zao waache tabia hiyo mara moja
kwamba inawaaibisha wanawake wote nchini ..
Nae
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda alieleza
licha ya jitihada zinazochukuliwa na Serikali kwa kushirikiana
na makundi mbalimbali ya kijamii ,takwimu bado ninaonnnyesha
ongezeko la ukatili wa kijinsia .
Alisema
ongezeko hilo linachangiwa na changamoto zifuatazo ambazo ni
imani za kishirikina ,mila na desturi za badhi ya makabila ,umasikini
, elimu na ukosefu wa nyumba salama ambapo baadhi ya wazazi
wamekuwa wakiwalaza wageni wao na watoto wao na kusababisha wageni hao kuwafanyia vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia .
0 comments:
Post a Comment