Na Walter Mguluchuma .
Chama cha Skauti Wasichana na Wanawake Tanzania GIRL GUIDES TANZANI kImezinduliwa rasmi Mkoaani Katavi na wito umetolewa kwa wasichana na wanaweke waweze kujiunga na chama hicho ili waweze kupanua uwelewa wao wa uzalendo na kuwa tayari kufanya kazi kwa manufaa yao na Taifa .
Uzinduzi wa Chama hicho ulifanyika hapo jana katika uwanja wa Shule ya Msingi Mpanda na kuhudguriwa na Wanafunzi wa Shule zote za Sekondari zilizopo katika Manispaa ya Mpanda ambapo mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo alikuwa ni Afisa Maendeleo wa Jamii wa Mkoa wa Katavi Anna Shumbi.
Katibu Mkuu wa Girs Guid Tanzania Grece Shaba alieleza kuwa Girls Guidedes kiulimwengu ilianzishwa mwaka 1910 na mwanzilishi wake alikuwa ni Lord Barden Powel wa Uingereza na Tanzania ilianzishwa Mwaka 1928 huko Kirimanjaro na mpaka sasa ipo katika mikoa 23 ya Tanzania .
Alisema chama hicho ni chama cha kujitolea na madhumuni yake ni kuwaendeleza wanawake pamoja na wasichana kijamii na kiuchumi kwa kuwapatia elimu na mafunzo kupitia kanuni za Girl Guides.
Mkufunzi wa Taifa Emeliana Stansilaus alisema lengo la chama hicho ni kuwapa nafasi wasichana na wanawake waweze kujifunza namna ya umiliki jamii na mazingira yake ili kuendeleza mali zao ,tabia inayokubalika na kumwezesha kuwa na ujasiri katika maamuzi yao .
Alisema chama hicho kipo wazi kwa wasichana na wanawake wote waliokubali kuapa na kufuata kanuni za chama hicho .
Wanachama wa Girl Guides wamegawanyika katika makundi ya umri mbalimbali miaka saba hadi viangaza kumi hadi kumi na tano Guides, kumi na sita hadi 25 Rangers 26 hadi 30 viongozi vijana na 31 ni viongozi wakubwa .
Mgini Rasmi kwenye uzinduzi huo Afisa Maendeleo ya jamii Mkoa wa Katavi Anna Shumbi aliwakata wasichana na wanawake wa Mkoa wa Katavi wahamasike kwa wingi na kujiunga na chama hicho .
Alisema uendapo watajiunga na Girl Guides wataeza kupanua uelewa wao wa kuwa wazalendo na kuwafanya wafanye kazi zao kwa manufaa yao na Taifa na pia wataongeza ukakamavu na uwezo wa kujitambua zaidi.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment