Thursday, November 23, 2017

GIRLS GUIDES YAZINDULIWA KATAVI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



Na  Walter Mguluchuma .
  Chama  cha   Skauti Wasichana na  Wanawake  Tanzania   GIRL  GUIDES  TANZANI  kImezinduliwa   rasmi   Mkoaani  Katavi  na  wito umetolewa  kwa  wasichana  na  wanaweke   waweze kujiunga na chama hicho ili waweze kupanua  uwelewa  wao wa uzalendo  na kuwa tayari kufanya kazi  kwa   manufaa yao   na Taifa .
 Uzinduzi wa  Chama  hicho  ulifanyika  hapo   jana    katika     uwanja wa   Shule ya  Msingi  Mpanda na kuhudguriwa  na  Wanafunzi wa  Shule  zote  za   Sekondari  zilizopo   katika  Manispaa ya   Mpanda   ambapo   mgeni  rasmi   kwenye  uzinduzi huo   alikuwa ni   Afisa   Maendeleo wa   Jamii  wa   Mkoa wa   Katavi   Anna  Shumbi.
Katibu  Mkuu  wa   Girs  Guid  Tanzania  Grece   Shaba   alieleza  kuwa  Girls  Guidedes kiulimwengu ilianzishwa  mwaka  1910 na  mwanzilishi wake    alikuwa ni   Lord   Barden  Powel wa  Uingereza  na   Tanzania  ilianzishwa  Mwaka  1928  huko  Kirimanjaro  na  mpaka  sasa  ipo  katika  mikoa 23 ya  Tanzania .
  Alisema    chama  hicho  ni  chama  cha kujitolea  na  madhumuni  yake  ni  kuwaendeleza  wanawake  pamoja   na  wasichana  kijamii na kiuchumi  kwa kuwapatia   elimu  na  mafunzo  kupitia  kanuni  za   Girl  Guides.
Mkufunzi  wa  Taifa   Emeliana    Stansilaus  alisema   lengo  la   chama  hicho  ni  kuwapa   nafasi  wasichana  na  wanawake  waweze   kujifunza    namna  ya umiliki   jamii na  mazingira yake  ili  kuendeleza  mali  zao ,tabia inayokubalika  na kumwezesha  kuwa  na ujasiri  katika  maamuzi yao .
 Alisema  chama  hicho  kipo  wazi  kwa   wasichana   na  wanawake   wote   waliokubali  kuapa  na kufuata  kanuni za    chama  hicho .
 Wanachama  wa  Girl   Guides wamegawanyika  katika  makundi ya  umri  mbalimbali   miaka     saba   hadi  viangaza   kumi  hadi  kumi  na  tano   Guides, kumi na  sita  hadi    25  Rangers   26  hadi   30  viongozi   vijana  na   31  ni  viongozi  wakubwa .
  Mgini   Rasmi  kwenye   uzinduzi  huo  Afisa    Maendeleo ya   jamii   Mkoa  wa  Katavi   Anna   Shumbi  aliwakata   wasichana na  wanawake wa  Mkoa  wa   Katavi   wahamasike kwa   wingi  na kujiunga  na   chama  hicho .
Alisema  uendapo  watajiunga  na  Girl  Guides  wataeza  kupanua  uelewa  wao  wa  kuwa  wazalendo  na  kuwafanya  wafanye  kazi  zao  kwa  manufaa  yao na  Taifa  na  pia   wataongeza  ukakamavu na  uwezo wa kujitambua zaidi.
MWISHO


No comments:

Post a Comment