Na Walter Mguluchuma
Katavi.
KATEKISTA wa
Kanisa katoliki Jimbo la Mpanda mkoani Katavi aliyekuwa akitoa huduma
za kiroho katika Kigango cha Mchakamchaka , Noel Sitemele amefikwa na
umauti muda mfupi baada kumaliza kuongoza ibaya ya mazishi ya muumini
wake juzi .
Kigango cha Mchakamchaka kipo kijiji ni Majalila katika Parokia ya Mpanda Ndogo katika wilaya ya Tanganyika mkoani humo.
Akisimulia tukio hilo Diwani wa Kata ya Mpanda ndogo Hamad Mapendo ambae pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.
alisema mwalimu huyo wa dini pia alikuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Majalila Halmashauri ya Mpanda Wilaya ya Tanganyika .
Alisema katekista huyo alifariki dunia juzi juzi , saa kumi na moja
jioni muda mfupi baada ya kufikishwa katika zahanati ya
Kijiji hicho kabla hata ya kuanza kupatiwa matibabu.
Alisema
kabla ya mauti hayaja mfika siku hiyo marehemu aliongoza ibada
ya mazishi kuanzia mwanzo wa ibada hadi mwisho wa ibada ya mama
mmoja ambae alikuwa amefariki dunia kwenye kigango hicho siku hiyo.
Mapengo
alieleza mara baada ya kumaliza mazishi ya mama huyo muda
mfupi uliofuata alianza kujisikia vibaya kiafya hari ambayo
ilimfanya aamue kurudi nyumbani kwake na kuwaacha waombolezaji
wengine waliokuwepo kwenye msiba huo.
Baada
ya kuwa amefika nyumbani kwake hali yake ilizidi kubadilika
ambapo aliomba msaada kwa majirani zake wa kupelekwa kwenye
zahanati ya kijiji hicho ambayo haiku mbali kutoka nyumbani kwake .
.
Alisema
marehemu huo alifikishwa kwene zahanati ya kijiji cha
Mchakamchaka ambapo wakati tabibu akiwa anataka kuanza
kumpatia huduma akawa amefariki dunia na kusababisha simanzi na
mshtuko mkubwa kwa waliokuwa wamemzindikiza .
Taarifa za kifo cha Katekista huyo ziliwafikia waombolezaji
walikuwepo kwenye msiba wa marehemu ambae alikuwa ametoka
muda si mrefu kuongoza ibada ya mazishi hari ambayo iliwafanya
waombolezaji wengine washindwe kuamini kama kweli katekista
huyo aliyeongoza mazishi kama kweli amefariki dunia .
Maziko ya Katekista
huyo yalifanyika jana katika makaburi ya Mchakamchaka ambapo
ibada ya mazishi iliongozwa na Padri Pascal Kipenye ambae ni
Paroko wa Parokia ya Mpanda Ndogo yalihudhuriwa pia na Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini Moshi Kakoso
No comments:
Post a Comment