Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma.
Katavi
MKAZI wa Mtaa wa Kawajense katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi , Nkondwa Sikazwa (78) ambaye alikuwapatwa na upofu kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita ameshindwa kumtambua mkewe wa ndoa na kumkataa kuwa amezeeka baada ya kutibiwa na macho yake kuwa na nuru kama awali .
Mzee Sikazwa alisema kuwa alipofuka kwa zaidi ya miaka kumi hadi hivi karibuni alipoanza kuona tena baada ya kutibiwa na madaktari wabobezi wa macho ambao walikuwa wakijitolea .
Alibainisha
hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini hapo ambapo
alisema kuwa alifunga ndoa mwaka 1959 na mkewe aitwae Evelanda katika
Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga , Parokia ya Chala iliyopo wilayani Nkasi .
“Miaka yote kumi niliyokuwa niemepofuka mke wangu Evelanda alikuwa akinihudumia lakini siku macho yangu yalipo pata nuru na kusababisha niweze kuona tena sikuweza kumtambua mke wangu kwa kuwa nilimmwona amukuwa ameshazeeka tofauti na nilivyokuwa nikimwona kabla ya kuwa kipofu miaka kumi iliyopita “ alisisitiza mzee Sikazwa .
Akisimulia masaibu yaliyompata alisema hivi karibuni walikuja madaktari bingwa wa macho Wajerumani waliokuwa wakijitolea katika Hospitali ya Manispaa ya Mpanda iliyopo mjini hapa na mie nlikuwa miongoni mwa wagonjwa wa macho tuliofika kutibiwa … nililipelekwa na binti yangu anayeishi katika kijiji cha Kakese “ alisimulia
Aliongeza kuwa baada ya kufanyiwa upasuaji wa macho yangu alifungwa bandeji machoni ambapo alishauriwa na daktari kutozifungua hadi zipite siku mbili ambapo alifanya hivyo .
“ Baada ya siku mbili kupita nilirudi tena kwa madaktari hao na mmoja wao alinifungua bandeji machoni hakika sikuamini kile kilichotokea kwani nilianza kuona tena baada ya miaka kumi kupita tangu nipofuke “ alieleza kwa bashasha kubwa .
Aliongeza kusema kuwa aliporejea nyumbani kwake alilakiwa na familia yake ambapo alitambulishwa kwa mkewe Evelanda hata hivyo alishindwa kumtambua na kumkata kuwa siye kwamba mkewe hawezi kuzeeka kiasi hicho .
“Hata hivyo baada ya kushauri na ndugu zangu kuwa Evelanda ndie mke wangu wa ndoa basi niliafiki na kukubali kuendelea kuishi nae kama mke wangu …… sio masihala heri mtu awe kiziwi lakini sio kuwa kipofu kwani mpaka nilishasahamu mke wangu aliyekuwa akinihudumia hadi unyumba kwa kipindi chote cha miaka kumi bila kunung’unika …alinivumilia sana kwa kipindi chote hicho
sasa tangu nimeanza kuona tena nalazimika kuzurura kwenye mitaa ya Mji wa Mpanda huku nikistaajabu mabadiliko makubwa ninayoyaona vitu vingi vimebadilika kwangu ni vigeni …. “ alieleza.
Alisema kuwa sasa kazi yake ni moja tu ambapo akishafungua kinywa anatembea mitaani hadi mchana ambapo anarejea nyumbani kula kisha anapumzika kidogo ambapo anaendelea tena na matembezi yake mitaani .
No comments:
Post a Comment