Home » » MZEE WA MIAKA 78 ALIYESHINDWA KUONA KWA MIAKA 10, SASA AANZA KUONA TENA

MZEE WA MIAKA 78 ALIYESHINDWA KUONA KWA MIAKA 10, SASA AANZA KUONA TENA

 PICHA YA   MZEE  NKONDWA  BAADA YA KUPONA UPOFU AKIWA ANALANDA LANDA KATIKA MTAA WA KAWAJENSEALI


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.



  Na Walter  Mguluchuma.
    Katavi


MKAZI wa Mtaa wa Kawajense katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi , Nkondwa Sikazwa (78) ambaye alikuwapatwa  na upofu  kwa zaidi ya miaka 10  iliyopita ameshindwa kumtambua mkewe wa ndoa na kumkataa kuwa amezeeka baada ya kutibiwa  na macho yake kuwa na nuru kama awali .

Mzee Sikazwa alisema kuwa alipofuka kwa zaidi ya miaka  kumi  hadi hivi karibuni alipoanza kuona tena  baada ya kutibiwa  na  madaktari wabobezi wa macho ambao walikuwa wakijitolea .

Alibainisha hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini hapo ambapo alisema kuwa alifunga ndoa mwaka 1959 na mkewe aitwae Evelanda katika Kanisa Katoliki  Jimbo la Sumbawanga , Parokia ya Chala iliyopo wilayani Nkasi .

“Miaka  yote  kumi  niliyokuwa niemepofuka  mke wangu Evelanda alikuwa akinihudumia lakini siku macho yangu  yalipo pata nuru na kusababisha niweze kuona tena  sikuweza kumtambua mke wangu kwa kuwa nilimmwona  amukuwa   ameshazeeka  tofauti na nilivyokuwa nikimwona kabla ya kuwa kipofu miaka kumi iliyopita “ alisisitiza  mzee Sikazwa .

Akisimulia masaibu yaliyompata alisema  hivi karibuni walikuja madaktari  bingwa wa  macho Wajerumani  waliokuwa  wakijitolea  katika  Hospitali ya Manispaa ya  Mpanda iliyopo mjini hapa  na  mie  nlikuwa  miongoni mwa wagonjwa wa macho tuliofika  kutibiwa … nililipelekwa na binti yangu anayeishi  katika kijiji cha Kakese “ alisimulia


 Aliongeza kuwa baada ya kufanyiwa upasuaji wa macho yangu alifungwa  bandeji  machoni ambapo alishauriwa  na  daktari  kutozifungua hadi zipite siku mbili ambapo alifanya hivyo .

“ Baada ya siku mbili kupita nilirudi tena kwa madaktari hao na mmoja wao alinifungua bandeji machoni  hakika sikuamini  kile kilichotokea kwani nilianza kuona  tena baada ya miaka  kumi kupita  tangu nipofuke “ alieleza  kwa bashasha kubwa .

Aliongeza kusema kuwa aliporejea nyumbani kwake alilakiwa na familia yake  ambapo alitambulishwa kwa mkewe  Evelanda  hata hivyo alishindwa kumtambua na kumkata  kuwa siye  kwamba mkewe  hawezi  kuzeeka kiasi  hicho .
 “Hata hivyo  baada ya kushauri na ndugu zangu  kuwa Evelanda  ndie mke wangu wa ndoa basi niliafiki na kukubali kuendelea  kuishi nae kama mke  wangu …… sio masihala  heri mtu awe kiziwi lakini sio kuwa kipofu  kwani mpaka nilishasahamu mke wangu aliyekuwa akinihudumia  hadi unyumba kwa kipindi chote cha miaka kumi bila kunung’unika  …alinivumilia sana  kwa kipindi chote hicho
sasa tangu nimeanza kuona tena  nalazimika kuzurura kwenye mitaa  ya Mji wa Mpanda huku nikistaajabu  mabadiliko makubwa ninayoyaona  vitu vingi vimebadilika  kwangu ni vigeni …. “ alieleza.
Alisema kuwa sasa kazi yake ni moja tu ambapo akishafungua kinywa anatembea mitaani  hadi mchana ambapo anarejea nyumbani  kula kisha anapumzika kidogo ambapo anaendelea  tena na matembezi yake mitaani .





0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa