Na Walter Mguluchuma.
Katavi .
Benki ya NMB imetenga zaidi ya Shilingi Bilioni Moja kwa ajiri ya kuchangia maendeleo ya Wananchi ikiwemo kusaidia sekta ya afya na Elimu kiasi hicho kinaifanya kuwa Benki ya kwanza hapa katika kuchangia maendeleo kuliko Benki yoyote hapa Nchini .
Hayo yalisemwa hapo jana na Meneja Mahusiano Biashara ya Serikali wa Benki ya NMB wa Kanda ya nyanda za juu Focus Lubende wakati wa hafla ya kukabidhi bati 300 kwa ajiri ya Shule ya Msingi Kilida Katika Halmashauri ya Mpimbwe na Kompyuta 7 kwa ajiri ya Shule za Sondari tatu za Halmashauri hiyo hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya ofisi ya Halmashauri ya Mpimbwe.
Alisema kwa mwaka huu wa 2017 NMB imetenga zaidi ya shilingi Bilioni moja kwa ajiri ya kuchangia maendeleo ya wananchi ikiwemo kusaidia sekta ya afya na elimu na kuifanya benki hiyo kuwa kuwa benki ya kwanza katika kuchangia maendeleo kuliko benki yoyote hapa nchini .
Focus alieleza kuwa NMB ndio inayoongoza nchini kwa kuwa na matawi mengi kwani inajumla ya matawi 217 na ATM zaidi ya 800 kwa nchi nzima pamoja na wateja zaidi ya milioni mbili ambayo ni hazina ambayo hakuna benki nyingine yenye inayo .
Alisema kwa miaka kadhaa sasa Benki hiyo katika mipango yake imekuwa ikishiriki shughuli mbalimbali za jamii kama kusaidia sekta ya elimu madawati na viti kwa upande wa afya wamekuwa wakisaidia vitanda magodoro na shuka .
Pia huwafariji jamii katika vipindi vya majanga mbalimbali zinazogusa maisha ya watu wengi baada ya kutambua kuwa kupitia jamii ndipo wateja wengi wanapo toka kwa hiyo kurudisha sehemu ya faida kwa jamii ni utaratibu wao .
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali mstaafu Raphael Muhuga aliiomba benki hiyo kufungua matawi kwenye maeneo ya Kata za Majimoto na Usevya Wilayani Mlele na Kasekese Wilayani Tanganyika kwani maeneo hayo yanamzunguko mkubwa sana wa fedha .
Alisema MNB ndio benki pekee inayotowa huduma za Kibenki katika Wilaya ya Mlele na imekuwa ikitowa misaada mbalimbali kwenye jamii katika maeneo ya Mkoa wa Katavi kira mara wanapokuwa wameombwa kufanya hivyo .
Nae Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda alisema msaada wa bati uliotolewa na benki hiyo utasaidia sana kwenye shule ya msingi Kilida iliyopata janga mwezi machi mwaka huu ya kuenzuliwa paa lake na hivyo kuwafanya wanafunzi kujifunza katika mazingira magumu.
Alisema Kompyuta saba walikabidhiwa wamepanga kuzigawa katika Shule tatu za Sekondai zilizopo katika Halmashauri hiyo ya Mpimbwe ambazo alizita kuwa ni Sekondari ya Mpinde ,Mamba na Usevya.
Katika tukio hilo la janga la mvua watu watu sita walifariki dunia baada ya kusombwa na maji na pia kulitokea uharibifu mkubwa wa nyumba za makazi ya watu na barabara.
No comments:
Post a Comment