FOCUS LUBENDE MENEJA MAHUSIANO BIASHARA WA BENKI YA
NMB KANDA YA NYANDA ZA JUU AKIMKABIDHI MKUU WA MKOA WA KATAVI
MEJAGENERALI MSTAAFU RAPHAEL MUHUGA KOMPYUTA 7 ZILIZOTOLEWA
MSAADA NA BANK YA NMB KWA AJIRI YA SHULE NNE ZA SEKONDARI ZA HALMASHAURI YA MPIMBWE WILAYANI MLELE MSAADA HUO ULIKABIDHIWA HAPO
JANA KWENYE HAFLA ILIFANYIKA KATIKA OFISI YA HALMASHAURI YA MPIMBWE
NA KUHUDHURIWA NA VIONGOZI KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WA MKOA WA KATAVI
NA WAWILAYA YA MLELE WALIONGOZWA NA MKUU WAO WA WILAYA YA MLELE RACHEL
KASANDA PAMOJA NA MADIWANI
Katavi .
Benki ya NMB imetowa msaada wa Bati 300 zenye thamani za Tshs 8,000,000 kwa ajili ya shule ya Msingi Kilida iliyoko katika Halmashauri ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi ambayo majengo ya madarasa ya Shule hiyo yalienzuriwa na mvua na Kompyuta 7 kwa ajiri ya Shule tatu za Sekondari kwenye Halmshauri hiyo .
Msaada huo ulikabidhiwa hapo kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali Mstafu Raphael Muhuga na Govemment Ralationship Manenger Meneja Mahusiano Biashara ya Serikali wa NMB wa Kanda za Nyanda za Juu Focus Lubende kwa niaba ya uongozi wa Benki ya Nmb katika Hafla iliyofanyika katika viwanja vya Halmashauri ya Mpimbwe.
Focus alisema uongozi wa Mkoa wa Katavi ulitambua kabisa kuwa NMB ni Benki iliyokaribu na Wananchi na hivyo kuwa ni sehemu ya kwanza ya kukimbilia ili kutatua changamoto ya majanga ya mvua yalioleta madhara makubwa katika Wilaya ya Mlele .
Wao kama NMB walipata maombi ya kuombwa msaada kupitia kwa Mkuu wa Wilaya ya Mlele walifarijika na kuamua mara moja kuja kushirikiana na Mkoa wa Katavi kunusuru maisha ya watu wakati wa janga la mvua zilizoharibu majengo na miundo mbinu mbalimbali katika Vjiji vya Kasansa na Kilida Wilayani Mlele .
Alishukuru kwa wao kutambuliwa kuwa NMB ni mahali sahihi ,hii inaonyesha thamani kwa kutambuliwa kwa michango yao wanayoitowa kwenye jamii kama benki inayochangia maendeleo.
Alisema vifaa hivyo walivyovikabidhi ni sehemu ya ushiriki wao katika maendeleo ya jamii na wao kama benki inayoongoza Tanzania kw a kuwa na matawi mengi wanahakikisha jamii inayowazunguka inafaidika kutokana na faida wanayoipata.
Wanafahamu kuwa Shule ya Msingi Kilida ilipata janga la kuenzuliwa paa lake la majengo ya madarasa hivyo kufanya mazingira ya wanafunzi kuwa magumu .
Alisema benki hiyo inatambua mabati hayo waliotowa yatarejesha tabasamu kwa wanafunzi ,walimu na jamii nzima ya Kilida na Mlele na kwa wanakazi wote kwa ujumla wake .
Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda alisema kuwa msaada huo wa bati utasaidia kurekebisha majengo ya madarasa yalioenzuliwa na mvua kali iliyonyesha mwezi machi mwaka huu na kusabisha vifo vya watu sita na miundo mbinu mbalimbali .
Pia aliishukuru NMB kwa msaada wa Kompyuta saba walizozitowa ambapo wao kama Wilaya wamepanga kuzipeleka kwenye Shule za Sekondari za Mamba ,Usevya na Mbende.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Raphael Muhuga alisema Nmb ndio Benki pekee inayotowa huduma za kibenki katika Wilaya ya Mlele na aliiomba benki hiyo ifungue matawi mengine kwenye Wilaya hiyo .
Aliyataja maeneo ambayo yanawatu wengi na mzunguko wa fedha ambayo yanasitahili kuwa na huduma za benki hiyo kuwa ni Maji moto na usevya katika Wilaya ya Mlele na Kasekese Wiyani Tanganyika .
MWISHO
No comments:
Post a Comment