Tuesday, October 24, 2017

JUMLA YA WATU ZAIDI YA 13,000 MKOANI KATAVI WANATUMIA DAWA YA ARVs.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Na  Walter  Mguluchuma .
        Katavi .
 Mkoa wa  Katavi hadi sasa  unajumla ya  wateja wapya  na wanaondelea  kutumia  dawa  za  ARVs   13,671  ambapo ni  sawa na  asilimia 56 ya watu  wote wanao  kisiwa kuwa  kuwa  na   maambukizi ya  VVU  katika   Mkoa wa  Katavi  huku Mkoa ukiwa umefanikiwa  kuongez vituo  vya tiba na   matunzo kutoka 11  hadi 20.
 Hayo yalisemwa  hapo  jana  na  Mganga   Mkuu wa  Mkoa wa   Katavi  Dr  Yahaya   Hussein wakati  alipokuwa  akosoma  taarifa fupi  ya  mradi wa  kuthibiti Ukimwi  Mkoa wa  Katavi wakati wa hafla  fupi ya kukabidhi   gari  moja   la  Manispaa ya   Mpanda  na  pikipiki  26 kwa  Halmashauri zote   tano za  Mkoa wa  Katavi  ikiwa ni  msaada    wa kutoka     water  red  Program    Tanzania   WRP   T   hafla iliyofanyika  katika  viwanja vya ofisi ya Mkuu wa  Mkoa wa Katavi .
 Alisema  kuanzia  mwezi  Januari 2017 kiasi cha wateja  waliotambulika  kuwa na maambukizi  ya VVU  na kufanikiwa  kuandikishwa  katika vituo  tiba  na mafunzo , jumla ya  wateja  4,212 walifanikiwa  kuunganishwa  katika  vituo vya  huduma  na  matunzo  hadi kufikia   30 Septemba   2017.
 Dr  Yahaya  alifafanua  kuwa  Mkoa wa  Katavi  unajumla ya  wateja  wapya  na wanaoendelea  kutumia   dawa ya   ARVs 13,671  sawa na  asilimia 56 ya watu wote  wanaokisiwa kuwa na  maambukizi ya  VVU .
Mkoa  utaendelea  kutekeleza   sera ya  Wizara ya  Afya kwa kuhakikisha asilimia 100 ya wajawazito wote wanahudhuria  kiliniki  ya akina mama wajawazito  pamoja na wanaonyonyesha  wote wanapimwa hari ya maambukizi  na wale wanaotambulika  kuwa na    maambukizi ya   VVU  wanaunganishwa katika  matibabu  ya ARVs  mara moja  ili kumkinga mtoto aliyezaliwa na  anaenyonya .
Alisema   pamoja  na   jitihada  kubwa    zinazofanywa   na watumishi  pamoja na timu  za usimamizi  wa huduma ya afya  ngazi ya  Mkoa  na  Halmashauri , Mkoa   bado   unakabiliwa  na  changamoto   mbalimbali    katika  kuendelea  kutimiza malengo waliyoyaweka  na  alizitaja baadhi ya  changamoto hizo kuwa ni .
Uhaba wa watumishi   katika  vituo  vya kutolea huduma   za CTC  ambavyo  vimeongezeka   kutoka kumi  na moja na kufikia  idadi ya vituo ishirini  vya huduma   tiba  na  mafunzo  kwa  Mkoa  mzima wa  Katavi .
Idadi   kubwa ya wateja  wanaopotea  katika  dawa  kutokana  na sababu    mbalimbali  ikiwemo  umbali  wa kufikia  kwenye  vituo  vya tiba  na  mafunzo ,shughuli za kilimo  na mifugo   zinachangia wateja  kuhama  bila kutowa taarifa  na kuonekana  kama wateja watoro .
 Alitaja  changamoto  yingine kuwa ni   shughuli za  udhibiti   UKIMWI   hazipewi  kipaumbele  cha kutosha  katika  kutenga   rasilimali  za  Halmashauri  husani magari  na  hivyo  kukwamisha   shughuli za  mradi  kufanyika kwa  wakati .
Mkuu wa  Mkoa wa  Katavi  Meja  Generali  Mstaafu  Raphael   Muhuga   alisema    Mkoa huo    unakabiliwa na  tatizo  la  maambukizi  ya VVU   hivyo  jitihada  kubwa   zinahitajika  ili  kuweza   kudhibiti maambukizi ya  VVU .
 Alisema   msaada wa  vitendea  kazi uliotolewa  na    WRP   T  usaidia  kuboresha  kazi  kwenye   Halmashauri za  Mkoa wa  Katavi  katika  swala zima la kuthibiti Ukimwi .
Mkurugenzi wa  Manispaa ya  Mpanda  Michael  Nzyungu  alisema  gari   moja walilopatiwa na pikipiki  nne  kwenye  Manispaa  hiyo  zitasadia  kupata taarifa na  mapema za  maambukizi ya  VVU  kutoka kwenye  vituo vya kutolea  huduma kwani   hawakuwa na  gari lata  moja  lililokuwepo kw  ajiri ya huduma hiyo .

No comments:

Post a Comment