Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Shirika la Water reed Program Tanzani WRP T limetowa msaada wa gari moja kwa Manispaa ya Mpanda na pikipiki 26 kwa Halmashauri za Mkoa wa Katavi wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 267 kwa ajiri ya shughuli za mradi wa kutdhibiti Ukimwi Mkoani Katavi .
Msaada huo ulikabidhiwa hapo jana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Gegerali Mstaafu Raphael Muhuga kwa Halmashauuri zote tano za Mkoa wa Katavi katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi .
Akiwa taarifa ya msaada huo Reginol Program Maneger WRP T wa Mkoa wa Katavi Dr Baraka Mgiriwa alisema msaada huo wa gari moja na pikipiki 26 umegharimu kiasi cha Tshs 267,789.707 milioni.
Alifafanua kuwa katika msaada huo Manispaa ya Mpanda wamepata gari moja aina ya Picup Land Cruzan a lenye thamani ya Tshs 168,987.707 Milioni pikipiki 4 aina ya Honda , Halmashauri ya Mpanda pikipiki 5, Mlele pikipiki 5, Nsimbo pikipiki 6, Mpimbwe pikipiki 5 na ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa pikipiki moja zikiwa na thamani ya Tshs 98,800,000.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr Yahaya Huseein alieleza kuwa baada ya Halmashauri kukabidhiwa msaada huo wanamatarajio makubwa ya kutowa huduma mbalimbali katika maeneo ya Halmashauri hizo alizitaja baadhi ya huduma hizo kuwa ni .
Kuimarika kwa shughuli za usarishaji wa sampuli kavu za damu za watoto waliozaliwa na mama wenye maambukizi ya VVU kwa ajiri ya kupimwa hali ya maambukizi .
Kupunguza uharibifu wa sampuli za damu kwa watoto waliozaliwa na mama wenye VVU pamoja na zile za kupima wingi wa kiwango cha vvu katika damu kwa WAVIU wote kwa kuchelewa kusafirishwa kwenda katika maabara.
Dr Yahaya alitaja matarajio megine kuwa ni kuongeza uchukuaji na usafirishaji wa sampuli za damu kwa ajiri ya kupima wingi wa VVU katika damu kwa WAVIU ili kuweka tiba sahihi kwa wale watakao kuwa na idadi kubwa ya kiwango cha vvu katika damu .
Pia wanatarajia kutekeleza shughuli zote zilizo hainishwa katika mpango kwa wakati na kwa haraka kwa kutumia vitendea kazi hivyo walivyo kabidhiwa na WRP..T.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Raphael Muhuga alisema kuwa msaada huo utasaidia sana kuboresha utendaji kazi kwa wagonjwa kupatiwa huduma kwa wakati tofauti na ilivyokuwa hapo awali .
Na alizisisitiza Halmashauri zote za Mkoa huo zione umuhimu wa kuvitunza vitendea kazi hivyo na wavitumie kwa makusudi yaliokusudiwa .
Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpimbwe Erasto Kiwale alisema kuwa kutoka na jografia ya Halmashauri yake pikikpiki hizo zitasaidia watumishi wa afya kwenda kutowa huduma kwenye maeneo ambayo hayafikiki kwa gari kwa urahisi .
Diwani wa Kata ya Mkanyagio Haidari Sumry alisema kuwa mapambano ya Ukimwi sio jambo dogo hivyo vitendea kazi hivyo hivyo vitasaidia wgonjwa kupa huduma kwa wingi kwa muda mfupi .
No comments:
Post a Comment