Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Chama cha Walimu Tanzania CWT wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi kimeiomba Serikali ipokee changamoto zinazowabili Walimu ambao ni wanachama wao na kuwapatia majibu yatakayo uonyesha utatuzi wa kero zinazowakabili Walimu .
Ombi hilo lilitolewa hapo jana kwenye risala yao kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Wilaya ya Mpanda uliofanyika katika ukumbi wa Mtakatifu Maria ilisomwa na Katibu wa CWT Wilaya ya Mpanda Wilson Masolwa.
Masolwa alisema Chama cha Walimu Tanzania CWT Wilaya ya Mpanda kinaiomba Serikali ipokee changamoto zinazowakabili Walimu ambao ni wanachama wa chama hicho na kuwapatia majibu yakakayo onyesha utatuzi wa kero zao .
Alieleza kuwa Chama cha Walimu kinataka kujua ni kwnini PSPF wanaendelea kukata fedha za kunua mgongo kwa walimu wastaafu ambao haikuwa jukumu lao kuwasilisha makato kwenye mfuko wa PSPF .
Kero nyingine waliitaja kuwa ni wastaafu kuendelea kucheleweshewa malipo yao ya kinua mgongo chao kipindi ambacho wanapokuwa wamestaafu na kuwaletea usumbufu walimu wo wastaafu .
Alisema Chama cha Walimu kinaiomba Serikali kuwasimamia waajiri wa mifuko ya Hifadhi ya Jamii kutowachelewesha walimu wastaafu kuwarudisha kwao mara tuu wanapo hitimu utumishi wao wa umma . kuanzia tarehe ya kustaafu na kama mifuko inapochelewesha malipo zaidi ya siku 60 na sababu za kuchelewesha malipo hazitokani na mstaafu mfuko ukubali kulipa tozo la asilimia 15 ya kiwango anachostahili kwa mwaka .
Mwenyekiti wa CWT Wilaya ya Mpanda Jumanne Msomba alieleza kuwa Chama hicho kimefanya mambo mengi hadi sasa kwa wanachama wake na kwa maendeleo ya ya sekta ya elimu .
Alitaja baadhi ya mambo ya maendeleo yaliofanya na chama hicho kuwa wameweza kuchangia mchango wa madawati 20 kwa shule ya msingi Mnyagala yenye thamani ya Tshs 2,500,000 saruji kwenye shule ya Msingi Kasekese na Sekondari ya Mpanda Ndogo yenye thamani ya Tshs 9,000,000.
Pia wamekuwa wakiwapatia bati 20 kwa kila mwalimu ambae anakuwa amestaafu na zoezi hilo huwa linafanyika kila mwaka bila kujari idadi ya walimu wanaokuwa wamestaafu kwa mwaka huo.
Na wamekuwa wakitowa motisha kwa Shule zilizofaulisha vizuri matokeo ya kidato cha sita na na darasa la saba pia wameweza kuwawezesha walimu 46 kupata viwanja vya makazi eneo la Mapinduzi Manispaa ya Mpanda .
Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Katavi John Mshoto aliwataka Walimu ambao ni wanachama wa Chama hicho kuacha kubaguana kati ya walimu wa Shule za Msingi na Sekondari .
Alisema kumekuwa na tabia ya walimu wa Sekondari na washule za Msingi kubaguana hata kwenye msiba kwa walimu hao pindi misiba inapokuwa imetokea jambo ambalo sio zuri zuri kabisa na halikubaliwi katika jamii.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa kwenye Mkutano huo ambae ni Mkuu wa Wilaya Tanganyika Salehe Mhando alisema kuwa Serikali inajitahidi kuhakikisha mazingira ya walimu yanakuwa mazuri .
Alisema matatizo waliyonayo walimu yatatatuliwa na Serikali kwa hatua kwa hatua na aliwaomba Walimu wamuunge mkono Rais John Magufuli katika jitihada zake za kusimamia raslimali za nchi kwani wanao nufaika na jitihada za Rais ni Wanzania wote.
Mkutano huu pia ulimchagua Lucas Izack kuwa mwakilishi wa walimu wenye ulemavu baada ya kupata kura 57 na kumshinda mgombea mwenzake kwenye nafasi hiyo Didas Kalonje alipata kura 44
MWISHO
No comments:
Post a Comment