Tuesday, October 10, 2017

CCM KATAVI WATENGUA MATOKEO YA MWENYEKITI WA WILAYA YA TANGANYIKA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na  Walter  Mguluchuma .
      Katavi .
Chama cha  Mapinduzi CCM   Mkoa wa  Katavi  kimetengua  matokeo ya  uchaguzi  kwa  nafasi  ya  Mwenyekiti wa   CCM  wa  Wilaya ya Tanganyika   na   nafasi ya  Katibu  wa   siasa na uenezi   pamoja na wajumbe wa  kamati ya siasa ya Wilaya  ambapo  Yasin  Kibiriti alikuwa  ameisha  tangazwa kuwa  Mwenyekiti   mpya wa  Wilaya hiyo  baada ya kubainika  msimamizi wa uchaguzi alikiika kanuni za uchaguzi .
 Uamuzi wa kufuta matokeo  hayo ya uchaguzi  ulitolewa  hapo  jana  na  kikao  maalumu  cha  kamati ya siasa  ya  Halmashauri kuu ya  CCM    Mkoa wa  Katavi  kilichofanyika  katika ukumbi wa   idara ya  Maji  kilichoongozwa na  Mwenyekiti wa  Ccm   Mkoa wa   Katavi   Mselemu   Abdallah.
Katibu  wa  Ccm wa  Mkoa wa  Katavi   Kajoro  Vyohoroka  aliwaambia wandishi wa  Habari jana ofisini kwake kuwa  kikao  hicho  kilipokea  malalamiko ya  uchaguzi   wa CCM  Wilaya ya Tanganyika kwa  nafasi ya  Mwenyekiti  wa Wilaya  ambapo uchaguzi wake ulifanyika  terehe 10 oktoba  na  Yasin Kiberiti  alitangazwa na   msimamizi  mkuu wa  uchaguzi huo    kuwa ndiye  mshindi.
 Alisema kikao  hicho  kilbaini  kuwa  ni  kweli  kwenye uchaguzi huo  kanuni  ya uchaguzi  ilikiukwa  na msimamizi  mkuu  wa uchaguzi   Crisant  Mwanawima  ambae   alikiuka  kanuni  ya uchaguzi  ya mwaka 2012 ibara ya 11b.
Aidha     ibara  ya  21  b  ya  kanuni inaeleza  wazi  kwamba   mshindi    katika uchaguzi  kwa wagombea wasio  kundini  lazima  mshindi  atakae  tangazwa  awe   amevuka  zaidi ya nusu  ya  kura  zote zilizopigwa .
Kajoro alifafanua kuwa  kwa matokeo  yaliotangazwa  siku  hiyo ya   msimamizi  mkuu wa   uchaguzi yalikuwa   yafuatayo  kura   zilizopigwa  zilikuwa 458 kura  halali  450 na kura  zilizoharibika  8 ambapo    Yasin  Kiberiti  alipata kura  222  Abdallah Sumry  kura  176 na  Mombo  Rashid  Mombo kura 55.
Alisema kwa   mantiki   hiyo  kikao  kiliamua  kutegua  matokeo yote ya uchaguzi  wa  CCM wa  Wilaya  ya  Tanganyika  kwa  nafasi ya    Mwenyekiti  wa  Ccm   Wilaya ,Katibu  wa siasa   na uenezi  wa  Wilaya  na wajumbe  wote  wa  kamati  ya siasa  ya Halmashauri  kuu ya Ccm  Wilaya.
Katibu  huyo wa  CCM   wa  Mkoa  alizitaja  sababu zilizopelekea  kutengua kwa matokeo ya  mshindi wa  Mwenyekiti wa  ccm  wa  Wilaya kuwa  ni  mshindi  kwenye uchaguzi huo hakupata zaidi ya nusu ya kura  halali  zilizopingwa  kwa mujibu  wa kanuni  ya uchaguzi .
Kwani Kikao kilichotengua matokeo hayo kilibaini kuwa   msimamizi mkuu  wa uchaguzi   kabla ya kutangaza  matokeo  hayo   yawezekana  alifanya  kwa makusudi  kwa lengo la kumbeba  mgombea  mmoja  na ndio maana  hakumshirikisha  msimamizi  msaidizi  wa uchaguzi  wala  mkurugenzi wa uchaguzi wa  wilaya  hiyo.
Alisema   kwakuwa   Mwenyekiti   alitangazwa   mshindi kinyume  na  kanuni   za  uchaguzi  ndani ya  chama   hivyo  hivyo  hata kikao cha   Halmashauri kuu  ya  Ccm   alichokiongoza baada ya kuchaguliwa  nacho kilikuwa ni  batili  hivyo matokeo ya  Katibu  na uenezi   pamoja  na  wajumbe wa   kamati ya siasa ya  Wilaya  nao  uchaguzi wao umefutwa.
Kuhusu  adhabu aliyopewa  msimamizi  huyo wa   uchaguzi   Kajolo  alisema   amepewa   adhabu  kwa mujibu  wa  kanuni za  chama  za uongozi  na maadili  kwa kushindwa  kwake  kusimamia  vema uchaguzi  huo  huku  akiwa   anajua  kuwa   anavunja    kanuni ya uchaguzi.
mwisho

No comments:

Post a Comment