Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Madiwani wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wametowa tamko la kumpongeza Rais John Magufuli kwa ujasiri aliouonyesha wa kulinda rasrilali za Nchi hasa katika swala la madini na wamawalaani vikali Watanzania wanaobeza jitihada hizo zinazofanywa .
Tamko hilo la madiwani lilitolewa hapo jana mbele ya Wandishi wa Habari na Meya wa Manispaa ya Mpanda Willy Mbogo kwa niaba ya Madiwani wote wa Manispaa ya Mpanda.
Mbogo alisema Madiwani wa Manipaa ya Mpanda wanatowa tamko la kumpongeza Rais John Magufuli kwa ujasiri mkubwa aliouonyesha wa kulinda rasilimali za nchi yetu na hasa katika suala zima la madini .
Alisema wanawalaani vikari Watanzania ambao wanaobeza jitihada hizo zinazofanywa na Rais za kulnda rasilimali zetu za Nchi za Madini kwa ajiri ya manufaa ya Wanzania wote .
Alieleza kuwa Rais mwanzo aliunda kamati mbili ambazo zilitowa taarifa na sasa amezifanyia kazi mapendekezo yaliotolewa na kamati hizo na tayari tumeanza kupata manufaa kwani Kampuni ya BARICK GOLD imekubali kutupatia ailimia 16 ya hisa za kampuni yao .
Na pia wamekubali kulipa Dola milioni mia tatu na kugawana nusu kwa nusu faida ya mapato yanayopatikana kitu ambacho kimetokana na jitihada za Rais wetu za kulinda rasilimali za Nchi yetu .
Alisema Madiwani wa Manispaa ya Mpanda wanaamini mapato hayo yatakayopatikana yataiongezea Serikali mapato na Halmashauri zitaongeza uwezo wa kutowa huduma kwa Wananchi wake .
Diwani wa Kata ya Makanyagio Haidari Sumry aliomba kuwa swala hilo lisiishie kwenye swala la madini tuu bali nguvu iongezeke kwenye maeneo mengine ili uchumi wa nchi uweze kukuwa na kuongezeka zaidi ya sasa.
Alisema endapo rasilimali za nchi zitasimamiwa vizuri Halmashauri zitanufaika na pato litakalokuwa limeongezeka Serikali kwani hata huduma kwenye Halmashauri zitaboreshwa zaidi .
Getruda Kabinda Diwani wa viti maalumu alisema kuna watu ambao walikuwa wakinufaika na ndio hao wanaobeza na kupinga jitihada zinazofanywa na Serikali za kulinda rasilimali za Nchi kwa faida ya Wanzania wote.
MWISHO
No comments:
Post a Comment