Na Walter Mguluchuma.
Katavi.
Naibu Waziri Waziri wa Nchi wa ofisi ya Rais Tamisemi George Kakunda amewataka Wa watumishi wa idara za Maliasili za Mkoa wa Kavi wawe makini katika utendaji wao wa kazi ili kulinda rasilimali za mistu ambazo zimekuwa zikisafirishwa kwa njia ya panya kwenda katika Mikoa mingine hapa Nchini .
Kakunda alitowa kauli hiyo hapo jana wakati alipokuwa akizungumza na viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Katavi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa w a Katavi wakati wa ziara ya siku moja Mkoani hapa .
Alisema Wizara yake inayotaarifa za utoroshwaji wa mazao ya Mistu kwa njia za panya kutoka Mkoani hapa kwenda katika Mikoa mingine unaofanywa na wafanya biashara kwa njia ya za panya na hasa nyakati za usiku .
Mazao ya mistu yanayotoroshwa sana bila vibali alitaja kuwa ni mbao ambazo zimekuwa zikisafirishwa kutoka Katavi na kupelekwa Mwanza bila kufuata utaratibu wa kulipia ushuru uliowekwa na Serikali .
Alisema inawezekana mazao hayo ya mistu yanayosafirishwa kwa njia za panya yakawa nanasafirishwa na wafanya biashara hao kwa kushirikiana na watumishi wa idara za maliasili ambao sio waaminifu .
Aliwaonya watumishi wanaofanya hivyo kushiriki kuhujumu rasimali za mistu kuwa kwa wale watakao bainika Serikali itawachukulia hatua kali za kinidhamu mara moja wakakapo kuwa wamebainika kushiriki kuhujumu rasilimali za za Nchi yetu .
Naibu Waziri huyo alisema ni vema watumishi wa Halmashauri wawe makini katika kufanya kazi za kulinda rasilimali za mazao ya mistu kwenye kila maeneo yao ili kuweza kuwadhibiti wanao hujumu rasilimali za mistu.
Pia alieleza kuwa Serikali inafikilia kujenga barabara za rami kwenye kila Halmashauri zote hapa Nchini kila mwaka kwani Halmashauri nyingi hapa Nchini makusanyo yao ya dani yanatofautiana baina ya Halmashauri na Halmashauri.
Alisema kwa sasa Serikali imesitisha utoaji wa urai kwa Raia wa Burundi kwa ajiri ya kufanya uhakiki kwa wale waliopewa urai wa Nchi ya Tanzania hivyo ni vema kwa wale raia wa Burundi ambao hawaja pewa urai wakadhibitiwa kwa kutotoka kwenye makazi mpaka wawe na vibali.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga alisema Mkoa wa Katavi unachangamoto kubwa ya upungufu wa watumishi wa kada mbalimbali kwa kiwango cha asilimia 35.
Muhuga alifafanua kuwa Sektarieti tuu ya Mkoa huo inao upungufu wa watumishi kwa asilimia 70 ya watumishi wote hari ambayo inasababisha hari ya utendaji kazi kuwa mgumu kutokana na idadi kubwa ya upungufu wa watumishi kwa ngazi ya Mkoa.
No comments:
Post a Comment