Na Walter Mguluchuma .
Katavi
NAIBU Waziri wa nchi Ofisi ya Rais , Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) , George Joseph Kakunda ameuagiza uongozi wa Serikali ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi kuwachukulia hatua kali ya kinidhamu na kijinai mara moja
ikiwemo kuwafukuza kazi walimu wanaofanya mapenzi na wanafunzi wao wa kike .
Naibu Waziri alielezwa kuwa walimu hao wamekuwa wakidai kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wao
ni sehemu ya ruzuku yao ya ualimu
Kufuatia tabia hizo za walimu hao Kakunda alitoa agizo hilo kwa viongozi wa Serikali ya Wilaya ya Mpanda alipokuwa
akizungumza na madiwani na watumishi wa Halmashauri ya Nsimbo akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja katika mkoa wa
Katavi .
Awali kabla agizo hilo halijatolewa , Diwani wa kata ya Katumba , Seneta Baraka alimweleza Naibu Waziri
Kakunda kuwa maisha yake yako hatarini
kutokana na kuwafuatilia kwa karibu walimu walio na mahusiano ya
kimapenzi na wanafunzi wao wa kike .
Aliongeza kuwa baadhi ya walimu wanaofundisha katika shule mbili za sekondari za Katumba na Kenswa zilizopo
katika makazi ya wakimbizi ya Katumba wamekubuhu katika kufanya mapenzi na wanafunzi wao wa kike huku wengine wakiwa wamewaoa
wanafunzi wao wakiwa bado hawajamaliza masomo yao .
“Baadhi ya walimu wanadai kuwa kufanya mapenzi na wanafunzi wao ni sehemu ya ruzuku yao ya ualimu ….. nimekuwa nikipata
ushirikiano hafifu na uongozi wa wilaya licha ya kutoa taarifa kwao zinazohusu tabia hizo za walimu hao
Hata hivyo uongozi wa wilaya umeshindwa kuwachukulia walimu hao hatua za kinidhamu na kijinai licha ya kuwepo ushahidi
wa kutosha Badala yake nimekuwa nikitishiwa maisha “ alisema.
Alimweleza
Naibu waziri kuwa yupo mwalimu mmoja anayefundisha kati ta shule hizo
mbili za sekondari ambaye ameamua kumuoa mwanafunzi wake wa kike ambaye
amelazimika kukatiza masomo
yake .
“Nilishatoa taarifa ya mwalimu huyu na wengine wenye
mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wao wa kike katika vikao vya baraza la madiwani lakini hakuna
hatua yeyote iliyochukuliwa dhidi yake baada yake baadhi ya madiwani
wenzangu wamevujisha siri za vikao na kwenda kuwataarifu
walimu hao kuwa mimi ndio ninaye washtakia” alieleza .
Alieleza kuwa mwalimu huyo baada ya penzi na mwanafunzi wake wa kike kukolea aliamua kuishi
kinyumba na mwanafunzi huyo hadi sasa ambapo tayari ameshalipa mahari
kwa wazazi wa msichana huyo .
Alisema kuwa hata hivyo mama mzazi wa msichana huyo amekataa katakata kupokea posa ya mwalimu huyo .
.Alimuomba Naibu Waziri amsaidie ili aweze kupatiwa ulinzi wa kutosha kwa kuwa maisha yake yako hatarini kutokana
na vitisho anayopewa kwamba hata siku hizi amelazimika kupunguza kutembelea maeneo ya starehe akihofia
maisha yake .
Mara
baada ya kupokea maelezo hayo Naibu Waziri Kakunda aliungiza
uongozi wa Serikali ya Wilaya ya Mpanda kuhakikisha inawachukulia
hatua kari ikiwemo kuwafukuza
kazi walimu wote watakao bainika kufanya mapenzi na wanafunzi kwa
kisingizio kuwa ndio ruzuku yao walimu kufanya mapenzi na walimu.
Alisema
sheria inakaza mtu kufanya mapenzi na mtoto mwenye umri chini
ya miaka 18 hivyo wanaofanya hivyo watambue kuwa wanafanya makosa na
wala hakuna mtu kusingizia kuwa
wlikubaliana .
Kakunda
alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha mtoto anasoma kuanzia
darasa la kwanza hadi kidato cha nne hivyo aliwaonya wanaowaozesha
wanafunzi wakae chonjo kwani
kufanya hivyo ni kosa kubwa .
Alizitaka
kamati za ulinzi na usalama za Kata hapa nchini zishirikiane
kufanya kazi ya kuhakikisha zinadhibiti mimba za wanafunzi kwenye
kata zao .
Afisa Elimu wa Sekondari wa Halmashauri ya Nsimbo Said Malamba alisema baadhi ya walimu wanaotuhumiwa
kufanya mapenzi na wanafunzi wao tayari wameisha anza kulishughulikia.
Alisema
na tayari walimu wawili wawili wa shule ya Sekondari Katumba
na mmoja wa Seokndari ya Kenswa walishaandikiwa barua na tume
ya utumishi ya kujieleza kutoka
na tuhuma hizo na baada ya kujieleza tayari Mwalimu Mmoja wa
Shule ya Msingi Katumba Mwalimu Fransis Manyala amechukuliwa
hatua na walimu wawili hawakupatikana na hatia.
Alisema
mwalimu huyo aliyepatikana na hatia kwenye tume ya utumishi ya
Wilaya ya Mpanda amekata rufaa kwenye tume ya utumishi ya Taifa
baada ya kutoridhika na maamuzi
ya kusimamishwa kwake kazi .
No comments:
Post a Comment