Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Wakazi wa Manispaa ya Mpanda Mkoani wamwlazimika kukosa huduma ya nyama ya Ng-ombe kwa muda wa siku moja baada ya kukosekana kwa huduma ya maji katika machinjio hari ambayo ilisababisha wafanya biashara wa kuuza nyama ya Ng-ombe kufunga Bucha zao .
Hari hiyo ya ukosefu wa nyama ya Ng-0mbe ilitokea hapo jana katika maeneo yote ya kwenye masoko ya Manispaa ya Mpanda na kuwasababishia wakazi wa Manispaa hiyo usumbufu mkubwa na kulazimika kununua mboga nyingine ambazo hawakuwa wamepanga kununua siku hiyo .
Mfanya biashara wa kuuza nyama ya Ng-ombe katika Bucha inayoitwa Bismilah iliyoko katika soko la Buzongwe Mjini hapa alisema wamelazimika kufunga bucha zao kwa siku nzima kutokana na kutokuwa na nyama ya Ng-ombe ya kuuza baada ya wafanya biashara kushindwa kuchinja mifugo yao kutokana na machinjio ynayomilikiwa na Manispaa ya Mpanda kukosa huduma ya maji machinjioni hapo .
Alisema siku hiyo ya jana walifika kwenye machinjio hiyo kama ambavyo huwa wanafika kwa lengo la kuchinja mifugo yao ya kuuza lakini walikuta machinjio hiyo haina huduma ya maji hari ambayo iliwalazimu kuanza kufatilia ilikujua tatizo hilo la ukosefu wa maji.
Nae mfanya biashara wa soko kuu la Manispaa ya Mpanda Juma Hassan alisema kuwa tatizo la ukosefu wa maji katika machinjio hiyo limekuwa likitokea mara kwa mara na limekuwa likijirudia .
Alifafanua kuwa tatizo hilo huwa linatokea mara nne au mara tano kwa kila mwezi na mara zote huwa wafanya biashara wana wamekuwa wakiambiwa waende wakachote maji na kuyabeba hadi kwenye machinjio kwa kutumia magari.
Chakushangaza jana afisa mifugo wa machinjio hiyo alikataa maji yasipelekwe kama amamekuwa wakitowa maji sehemu nyingine pindi machinjio hiyo inapokuwa imekosa maji .
Kwa upande wake Maneno Daniel mfanya biashara wa Bucha ya kuuza nyama ya Ng-ombe katika soko la Kachoma alieleza kuwa wao wamekuwa wakilipa ushuru kwenye machinjio kwa kila Ng-ombe anae chinjwa wanalipa ushuru wa Tshs 5000 na kila siku wanachinja Ng-ombe 50 sasa wao wanashangaa kwanini maji yakosekane wakati wo wanalipa ushuru.
Salome John Mkazi wa Kawajense Mjini hapa alisema alilazimika kutembea kwenye masoko zaidi ya matatu jana kutafuta nyama hata hivyo alfanikiwa kupata nyama ambayo ilikuwa imelala ambayo ilikuwa ikiuzwa katika bucha pekee inayoitwa Makololo katika soko la Buzongwe.
Meya wa Manispaa ya Mpanda Willy Mbogo alisema tatizo hilo wahusika ni MUWASA ambao hawako chini ya Manispaa wako chini ya Wizara ya Maji hivyo wao kama Manispaa wanashindwa kuwasimamia.
Endapo wangekuwa chini yetu sidhani kama kungekuwa na tatizo hilo mara kwa mara na pia bodi inayowasimamia mamlaka na Maji safi na maji taka MUWASA inaonekana haija kutana muda mrefu na ndio sababu watu wanafanya kazi wanavyo taka alisema Meya.
0 comments:
Post a Comment