Na Walter Mguluchuma.
Katavi .
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameipandisha hadhi Zahanati ya Inyonga kuwa Hospitali ya Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi baada ya kuikagua na na kuridhishwa na sifa za kuifanya kuwa Hospitali ya Wilaya.
Mwalimu aliipandisha Zahanati hiyo kuwa hospitali ya Wilaya hapo jana mara baada ya kuikagua na kuridhishw na vigezo vinavyo takiwa vya kuipandisha hadhi Zahanati hiyo kuwa Hospitali ya Wilaya .
Alisema ameamua kuipandisha hadhi zahanati hiyo kuwa Hospitali ya Wilaya kutokana na mamlaka aliyonayo kama Waziri wa Wizara husika.
Alivitaja baadhi ya vigezo vinavyofanya Hospitali iwe na hadhi ya Hospitali ya Wilaya kuwa ni huduma ya upasuaji , Chumba cha kuhifadhi maiti , maabara , huduma ya maji,umeme wa uhakika na huduma ya damu .
Alifafanua kuwa kama zahanati hiyo inatowa huduma kama hospitali ya Wilaya kwanini yeye kama Waziri mwenye dhamana ashindwe kuipandisha hadhi Zahanati hiyo na ukiangalia pia Wilaya hiyo haina Hospitali hata moja ya Wilaya .
Mwalimu alisema Rais John Magufuli Alisha waagiza Mawaziri kuwa na uamuzi wa kutowa maamuzi magumu pale panavyositahili kama ambavyo alivyofanya yeye kuipandisha hadhi Zahanati hiyo kwani .
Na alitowa ahadi ya kupeleka wataalamu wa Afya haraka iwezekanavyo wenye hadhi ya kufanya kazi kwenye Hospitali hiyo haraka iwezekanavyo kabla ya mwezi wa Septemba hauja kwisha .
Waziri huyo alikabidhi kwa niaba ya Rais magodoro 20 na ,vitanda 20 shuka 50 na vitanda vitano vya kisasa vya kujifungulia akina mama wajawazito kwa kwa ajiri ya Hospitali hiyo ya Wilaya.
Nae Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele DR Luccy Kafumu alieleza kuwa mchakato wa maombi wa kuipandisha hadhi zahanati hiyo ulianza toka mwaka 2013 baada ya wao kuona inasitahili kuwa Hospitali ya Wilaya .
Dr Kafumu alieleza kuwa Zahanati hiyo kwa muda wote toka mwaka 2013 imekuwa itowa huduma kama Hospitali ya Wilaya kwa kitendo hicho cha kuipandisha hadhi kitasaidia hata hela za kununua dawa kuongezeka kwenye bajeti ijayo
0 comments:
Post a Comment