Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii Jinsia , Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameziagiza Halmashuri zote hapa nchini kuhakikisha zinajenga vituo vya Afya kwa kuzingatia geografia ya eneo husika na kuangalia sehemu ambayo wanaishi watu wengi .
Agizo hilo alilitowa hapo jana wakati alipokuwa akizungumza na viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Katavi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Serikali za Mkoa huo.
Alisema Serikali inampango wa kujenga zahanati kwenye kila kijiji na Kituo cha Afya kwenye kila Kata ila kwa sasa ni vigumu kwa kila Kata kuwa na kituo cha Afya kutokana na uhaba wa wataalamu wa afya .
Hivyo kila Halmashauri iangalie uwezekano wa kufanya kila Kata tatu kuunganisha nguvu ya pamoja na kujenga kituo cha afya kimoja ambacho kitatowa huduma kwa wananchi w kata hizo tatu na waangalie geografia ya eneo husika na pia idadi ya wingi wa watu.
Alionya kuwa ipo tabia ya baadhi ya madiwani watakao taka kituo kijengwe kwenye Kata yake hata kama Kata nyingine ndio inayokuwa inasitahili hivyo ni vema wakaa pamoja madiwani na wataalamu wakashauliana kwanza sehemu ambayo inafaa kujengwa kwa kituo cha Afya.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Katavi Meja Generali mstaafu Raphael Muhuga alieleza kuwa vituo vya kutolea huduma za Afya vimeongezeka kutoka 72 kwa mwaka 2012 hadi vituo 84.
Alisema ili kutekeleza azma ya Serikali ya kila Kijiji kuwa na Zahanati Kata kuwa na kituo cha Afya na Wilaya kuwa na Hospitali ya Wilaya Mkoa wa Katavi katika kutekeleza mpango wa maendeleo ya Afya ya Msingi MMAM imejenga zahanati 21 toka mwaka 2012 hadi june 2017 hivyo idadi kuongezeka kutoka 59 hadi kufikia Zahanati 70.
Nae Asifa maedeleo ya Jamii wa Mkoa w Katavi Anna Shumbi alieleza kuwa Mkoa huo unakabiliwa na changamoto kubwa ya mimba za utotoni na kuufanya Mkoa huo kuwa ni miongoni mwa Mikoa inayoongoza kwa tatizo la mimba za utotoni .
0 comments:
Post a Comment