Walter Mguluchuma . Na Irine Temu
Katavi .
Wamiliki na madreva wa bajaji wanao fanya shughuli za usafiri katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamefanya mgomo na kusitisha kutowa huduma za usafiri katika maeneo ya Manispaa ya Mpanda na nje ya Manispaa baada ya SUMATRA kUpiga marufuku bajaji zote kufanya safari kwa kupitia barabara kuu.
Mwenyekiti wa wa madreva wa Bajaji Rashid Juma alisema wameamua kusitisha kutowa huduma ya usafiri kwenye maeneo ya Manispaa ya Mpanda na nje ya Manispaa baada ya Mamlaka ya usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA kupiga marufuku bajaji zote kufanya safari zake kwa kutumia barabara kuu zilizopo katika Mkoa wa Katavi .
Alisema wameamua kusitisha huduma hiyo ya usafiri kuanzia Agosti 7 ingawa SUMATRA lIkuwa imepatowa agizo hili lianze kutumika Agosti 8 hivyo wamesitisha huduma hiyo sio kwenye barabara kuu tuu bali wamesitisha kutowa huduma kwenye maeneo yote hata yale ya barabara ndogo mpaka hapo Sumatra itakapo waruhusu kutumia barabara kuu.
Mwenyekiti huyo alieleza kitendo cha kuwazuia kufanya safari kupia kwenye barabara kuu kutawafanya wakose mapato na kusabisha kushindwa kulipa mapato kwenye Mamlaka ya mapato hari ambayo itawza kuwafanya madreva hao kujiingiza kwenye maswala ya uharifu .
Mwenyekiti wa wasafirishaji ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya usalama barabarani wa Mkoa wa Katavi Nassor Arfi alisema ameisha pata taarifa za kusimamishwa kwa huduma za usafiri wa bajaji kupita kwenye barabara kuu za Mpanda Kigoma , Mpanda Sumbawanga na Mpanda Tabora na amefanya mawasiliano na Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambae amemwahidi kumpatia majibu baada ya kuwa amefanya mawasiliano na viongozi wa SUMATRA.
Arfi alisema Mkoa wa Katavi hau njia nyingine mbadala za kuwafanya madreva wa majaji kuweza kutumia hivyo ni vema SUMATRA wakatumia busara kwenye swala hilo kulingana na mazingira yalivyo kwa sasa katika Manispaa ya Mpanda.
Meneja wa SUMATRA wa Mkoa wa Katavi Amani Mwakalebela alieleza kuwa Nchi ya Tanzania inaendeshwa kwa kanuni na sheria na wao Sumatra wanafanya kazi kwa msingi wa sheria na kanuni na wao wametumia kifungu 18 cha sheria za usalama barabarani kuzizuia bajaji kupita kwenye barabara kuu.
Alisema pia wameangalia hali ya usalama kwa sasa baada ya barabara kuu kuwa za kiwango cha lami kumefanya usalama kwa sasa sio salama kwa bajaji kwa hivyo msimamo wa SUMATRA Mkoa wa Katavi ni bajaji zote kupita kwenye barabara ndogo na sio barabara kuu.
Aglipina Petro Mkazi wa mtaa wa Kazima alisema ameshindwa leo kumpeleka mgonjwa wake hospitali baada ya kukosa huduma ya usafiri wa Bajaji
Joice Longino Mkazi wa Kijiji cha Ibindi alieleza kuwa kitendo cha bajaji kusitisha huduma ya usafiri kumesababisha badhi ya wafanya biashara kushindwa kufika mjini Mpanda kununua bidhaa kwa ajiri ya biashara zao .
0 comments:
Post a Comment