Na Walter Mguluchuma.
Katavi .
Diwani wa Kata ya Kazima Manispaa ya Mpanda Elias Mwanisawa amelalamikia kitendo cha Wakazi wa Kata ya Kazima ambao wanazaidi ya miaka mitano sasa wameshindwa kulipwa fidia yao ya fedha kutokana na eneo lao la ekari 500 kuchukuliwa kwa ajiri ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha kilimo cha Mkoa wa Katavi ambacho kimeshindikana kujengwa .
Akitowa malalamiko hayo hapo jana mbele ya wandishi wa habari alisema jumla ya wakazi 200 wa Kata hiyo wanaidai Manispaa ya Ekari zao 500 zilizochukuliwa na Halmashauri hiyo kwa ajiri ya ujenzi wa Chuo kikuu cha Kilimo KUWA.
Mwanisawa alieleza kuwa Halmashauri ya Mji wa Mpanda sasa Manispaa walichukua eneo hilo la wakazi hao ambao walikuwa wakifanyizia shughuli mbali mbali zikiwemo za kilimo kwa lengo la kujenga chuo hicho cha kilimo ambacho kimeshindikana kujengwa baada ya kukosa wafadhili.
Alisema pamoja na ujenzi wa chuo hicho kuwa umeshindikana lakini Halmashauri ya Manispaa imeshindwa kuwarejeshea eneo lao hilo la ekari 500 baada ya hati miliki ya eneo hilo kuonekana mmiliki wa eneo hilo ni Manispaa licha ya kutokuwa wamelipa fidia kwa wananchi waliokuwa wakimiliki eneo hilo .
Alimwomba Rais John Maguful aingilie swala hilo kwani limekuwa ni lamuda mrefu sasa na limeshindwa kupatiwa ufumbuzi na viongozi wa ngazi ya Wilaya , Mkoa na Wizara ya Ardhi.
Nae Salome Pesambili alieleza kuwa kwa kuwa wameshindwa kulipwa fidia waliokuwa wameahidiwa kulipwa baada ya kuwa wamekubali kuacha maeneo yao ya ARDHI kwa ajiri ya kupisha ujenzi wa chuo hicho na kimeshindikana kujengwa huku wao wakiwa hawajalipwa fidia yao basi wanaomba warudishiwe ardhi yao .
Alisema yeye kama kiongozi wa wahanga hao aliwahi kwenda Dodoma mara mbili akiwa na baadhi ya wahanga wenzake na kuonana na Naibu Waziri wa Ardhi lakini mpaka sasa utekelezaji wa swala hilo hauja tekelezwa .
Said Juma alisema eneo hilo kabla ya kuchukuliwa na Halmashauri walikuwa wakilitumia kwa ajiri ya kuendeshea kilimo na waliweza kupata fedha za baada ya kuuza yao na waliweza kuwasomesha watoto wao shule .
Kumekuwepo na mgongano kwa muda mrefu sasa baina ya Halmashauri na wakazi hao ambao wamekuwa wakidai kulipwa fidia yao au kurudishiwa ardhi yao hata hivyo imekuwa ikishindikana kulipwa fidia ya ardhi yao kutokana na Halmashauri kutokuwa na fedha za kuwalipa fidia huku hati ya eneo hilo ikiwa ipo mikononi mwa Benki moja ambako iliwekwa kama mdhamana wakati wa taratibu zilipokuwepo za ujenzi wa chuo hicho Kikuu.
0 comments:
Post a Comment