Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Jumla
ya bunduki 395 na risasi 1478 na magazine mbili zimekamatwa kwa kipindi
cha mwaka mmoja kupitia doria za kukabiliana na ujangili zinazofanywa
na wizara ya maliasili na utalii katika hifadhi za taifa na mapori ya
akiba nchini huku watuhumiwa 472 wakifungwa vifungo virefu jela kwa
ujangili na wengine 469 wakitozwa faini ya zaidi ya shilingi milioni
452.
Akitoa
taarifa ya utendaji wa wizara hiyo waziri wa maliasili na utalii
Profesa Jumanne Maghembe anasema mafanikio hayo yanatokana na doria laki
tatu na nusu zilizofanyika nchi nzima ambapo mauaji ya Tembo yamepungua
kwa asilimia 45 huku changamoto kubwa ambayo bado inaikabili sekta hiyo
ni uingizwaji wa mifugo kwenye maeneo yaliyohifadhiwa.
Twaha
twaibu ni afisa uhusiano wa mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori nchini
tawa ambaye anasema kwa kipindi kifupi tangu mamlaka hiyo kuanza
kusimamia sekta ya wanyamapori matukio ya uijangili yamepungua huku
ikolojia ikionyesha idadi ya wanyama kuongezeka
0 comments:
Post a Comment