Na Walter Mguluchuma wa Katavi yetu Blog
Katavi .
Mahakama kuu Kanda ya Sumbawanga imemuhukumu Yustine Robarti 32 Mkazi wa Kijiji cha Maji Moto Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi kunyongwa hadi kufa baada ya kapatikana na hatia ya kumuua mke wake na watoto wake wadogo wawili na kisha kuwatumbukiza ndani ya kisima cha maji .
Hukumu hiyo ilitplewa hapo jana na Jaji wa Mahakama kuu Kanda ya Sumbawanga Adam Mambi katika vikao vya Mahakam kuu vinavyoendelea kufanyika katika mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi baada ya Mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo na upande wa mashitaka uliokuwa ukiongozwa na Mwanasheria mkuu wa serikali wa Mkoa wa Katavi Achiles Mulisi
Awali katika kesi hiyo mwendesha mashtaka Mwanasheria
mkuu wa serikali wa mkoa wa katavi alidai mahakamani hapo kuwa
mshtakiwa alitenda kosa hilo hapo Mach 23 mwaka 2015 majira ya saa 7 za
usiku baada ya kutokea ugomvi baina yake na mke wake wakati wakiwa wamelala chumbani na watoto wao wadogo ambao na hoa aliwaua pia.
Ilidaiwa kuwa siku hiyo ya tukio Yustini alimpiga mke wake aitwaye Monica Lwiche mwenye umri wa miaka 25 na kisha baada ya kumuuwa alimtupia katika kisima cha maji na pia aliwauwa watoto
wake wawili Eliza Robert mwenye miaka mnne na Frank Robart mwenye miaka
sita kwa lengo la kuvuruga ushahidi kwakuwa wakati akifanya kitendo
hicho watoto wake walikuwa wakishuhudia
Kabla ya kufanya tukio hilo mshtakiwa alikuwa ameisha toa kauli za vitisho kuwa endapo mke wake atarudi nyumbani atafanya jambo litakalokuwa la kihistoria na ambalo halitasahaulika kwa wakazi wa kata hiyo.
Mshtakiwa katika kesi hiyo alikuwa anatetewa na
wakili Patrick Mwakyusa ambapo upande huo wa utetezi ulikuwa na
mashahidi wawili mshtakiwa mwenyewe na Baba yake mzazi ambapo katika
utetezi huo waliiomba mahakama imwachie huru kwani upande wa mashtaka
umeshinda kudhibitisha kama kweli alitenda kosa hilo.
Pia upande huo wa utetezi ulidai kuwa upande
wa mashtaka umeshindwa kudhibitisha kuwa wakati anafanya mauaji hayo
hakuna mtu yoyote aliyeshuhudia tendo hilo la kumuuwa mke wake na watoto
na kuwatupia katika kisima cha maji.
Utetezi huo ulipingwa vikali na mwanasheria wa serikali Achiles Mulisi wa kile alichodai kuwa wakatika ugomvi huo unatokea mwanzoni mama mwenye nyumba alikokuwa amepanga mshtakiwa alishuhudia ugomvi huo na ushahidi wa maneno
ya vitisho aliyoyatoa mshtakiwa ni ushahidi tosha kuwa ndiye
aliyetekeleza mauaji hayo na kitendo cha kuwaua watoto nwake wawili
wanaojua kuongea na kumwacha mdogo aliyeokotwa barabarani ni ushahidi tosha.
Akisoma hukumu hiyo Jaji Adam Mambi aliiambia
mahakama kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande
wa mashtaka na utetezi Mahakama lazima iangalie mambo matatu ambayo ni ushahidi wa mazingira,je upande wa mashtaka unadhibitisha na kama kweli mshtakiwa amehusika katika mauaji hayo au la.
Hivyo aliieleza mahamakama kuwa kutokana na
maswali hayo matatu ambayo mahakama ilihoji ilidhika na ushahidi
uliotolewa na upande wa amshtaka na hivyo kumtia hatiani mshtakiwa
Yustin Robert kwa kosa la kifungu cha sheria namna 196 na 197 cha kanuni
ya adhabu na alitoa nafasi kwa mshtakiwa kujitetea kabla ya kusoma
hukumu.
Wakili wa mshatakiwa Patrick Mwakyusa allambia mahakama kutona na mshtakiwa kupatikana na kosa chini ya kifungu hicho cha sheria ambayo adhabu yake ni nmoja tu hana kiti chochote cha kuiomba mahakama .
Naye Mwasheria wa serikali aliiomba mahakama itoe
adhabu kali li iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hiyo na hasa
wanaowauwa watu wasikuwa na hatia na kutokana na mauaji kuwa mengi
mkoani katavi hasa kwa wanawake ni vyema mahakama ikatoa adhabu kali kwa
mshtakiwa huyo
Baada ya maelezo hayo Jaji Adam Mambi alisoma
kuhumu na kuieleza mahakama kuwa mshtakiwa Yustini amepatikana na hati
ya kuuwa watu watatu hivyo Mahakam imemuhukumu kunyongwa hadi kufa.
0 comments:
Post a Comment