Tuesday, July 18, 2017

TRL WALIOVAMIA HIFADHI YA RELI WATAKIWA KUONDOKA KWA HIYARI YAO VINGINEVYO NYUMBA ZAO KUBOMELEWA NA GHARAMA HIZO WATALIPISHWA WENYE NYUMBA WENYEWE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na    Walter    Mguluchuma
             Katavi

SHIRIKA la Reli Tanzania (TRL)  limewataka wananchi wote waliovamia
hifadhi za reli  na kujenga makazi  ya kuishi ya kudumu kuzibomoa
nyumba hizo  mara moja tena kwa hiyari yao  na kwa gharama zao wenyewe
..

Agizo hilo limetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Masanja Kadogosa
alipokuwa akizungumza na watumishi wa shirika hilo katika stesheni  ya
reli iliyopo katika Mji wa Mpanda katika mkoa wa Katavi .


  Alionya kuwa shirika hilo kamwe halitamwachi mtu yeyote aliyejenga
nyumba yake ndani ya hifadhi ya reli  na kuendelea kuishi  kwenye
makazi hayo  baada ya muda  uliotolewa wa miezi sita  kwisha ambao
uliwataka kuhama .
.

“Endapo baada ya muda wa miezi sita ukipita mtu yeyote ambaye atakuwa
amekaidi kubomoa nyumba yake Shirika litabomoa  na gharama zote
atatakiwa kuzilipa ….sasa kwa yale maeneo ambayo shrike litaamua
kupitia reli  kwenye makazi  ya watu hao ndio pekee watakaolipwa fidia
na shirika na si vinginevyo “ alionya .

Alisema amelazimika kutoa agizo hilo  kwa kuwa hivi karibuni shirika
hilo lilitoa notisi  ikiwataka watu waliojenga nyumba zao za makazi
katika maeneo ya Msasani na Tambuka Reli  katika Manispaa ya Mpanda
pamoja na wakazi wa kijiji cha Ugala  wilayani Mpanda  kubomoa nyumba
hizo ndani ya  kipindi cha siku 30 ..
Hata hivyo wakati wa ziara ya naibu waziri wa ujenzi na mawasiliano ,
Edwin Ngonyani aliyoifanya  mkoani Katavi aliwaongezea muda  wakazi
hao hadi Januari mwakani



Nae   Mwenyekiti wa  Bodi ya  Wakurugenzi ya  TRL      Prof       John
 Kondoro   aliwataka  watumishi  wa  TRL     wawe  wawazi  kila
wanapofanya  kazi  za  kuwahudumia  wananchi wao   kama   ambavyo
anavyofanya  kazi  Rais   John   Magufuli   ambavyo    hataki  njia
za     mkato  za  kufanya  kazi kwa  ujanja  ujanja .

  Alisema   shirika  hilo   halitakiwi kuwa   mzigo wa  Serikali
badala  yake    TRL   wao  ndio  wanatakiwa  kutowa   ruzuku  kwa
Serikali .

Mbunge  wa   Jimbo   la    Nsimno   Richald   Mbogo   alieleza  kuwa
 tayari   wananchi   wake   wa    Kijiji  cha   Ugala mameanza
kupimiwa   viwanja  kwa     ajiri  ya  ujenzi  wa  nyumba   zao  ili
waweze  kuhama   kwenye   maeneo ya    Hifadhi ya   Reli .

Alisema  yeye   kama    Mbunge  wa   Jimbo  la  Nsimbo    ameisha
andika  barua  ya  kumwomba  Waziri  wa  ujenzi  kuwaongezea  muda
wananchi    waliokuwa   wamejenga  nyumba  kwenye   maeneo  hayo
aliwaweze  kufanya   maandalizi ya  ujenzi  kwenye  maeneo
waliotengewa .

No comments:

Post a Comment