Na Walter Mguluchuma
Katavi
SHIRIKA la Reli Tanzania (TRL) limewataka wananchi wote waliovamia
hifadhi za reli na kujenga makazi ya kuishi ya kudumu kuzibomoa
nyumba hizo mara moja tena kwa hiyari yao na kwa gharama zao wenyewe
..
Agizo hilo limetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Masanja Kadogosa
alipokuwa akizungumza na watumishi wa shirika hilo katika stesheni ya
reli iliyopo katika Mji wa Mpanda katika mkoa wa Katavi .
Alionya kuwa shirika hilo kamwe halitamwachi mtu yeyote aliyejenga
nyumba yake ndani ya hifadhi ya reli na kuendelea kuishi kwenye
makazi hayo baada ya muda uliotolewa wa miezi sita kwisha ambao
uliwataka kuhama .
.
“Endapo baada ya muda wa miezi sita ukipita mtu yeyote ambaye atakuwa
amekaidi kubomoa nyumba yake Shirika litabomoa na gharama zote
atatakiwa kuzilipa ….sasa kwa yale maeneo ambayo shrike litaamua
kupitia reli kwenye makazi ya watu hao ndio pekee watakaolipwa fidia
na shirika na si vinginevyo “ alionya .
Alisema amelazimika kutoa agizo hilo kwa kuwa hivi karibuni shirika
hilo lilitoa notisi ikiwataka watu waliojenga nyumba zao za makazi
katika maeneo ya Msasani na Tambuka Reli katika Manispaa ya Mpanda
pamoja na wakazi wa kijiji cha Ugala wilayani Mpanda kubomoa nyumba
hizo ndani ya kipindi cha siku 30 ..
Hata hivyo wakati wa ziara ya naibu waziri wa ujenzi na mawasiliano ,
Edwin Ngonyani aliyoifanya mkoani Katavi aliwaongezea muda wakazi
hao hadi Januari mwakani
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRL Prof John
Kondoro aliwataka watumishi wa TRL wawe wawazi kila
wanapofanya kazi za kuwahudumia wananchi wao kama ambavyo
anavyofanya kazi Rais John Magufuli ambavyo hataki njia
za mkato za kufanya kazi kwa ujanja ujanja .
Alisema shirika hilo halitakiwi kuwa mzigo wa Serikali
badala yake TRL wao ndio wanatakiwa kutowa ruzuku kwa
Serikali .
Mbunge wa Jimbo la Nsimno Richald Mbogo alieleza kuwa
tayari wananchi wake wa Kijiji cha Ugala mameanza
kupimiwa viwanja kwa ajiri ya ujenzi wa nyumba zao ili
waweze kuhama kwenye maeneo ya Hifadhi ya Reli .
Alisema yeye kama Mbunge wa Jimbo la Nsimbo ameisha
andika barua ya kumwomba Waziri wa ujenzi kuwaongezea muda
wananchi waliokuwa wamejenga nyumba kwenye maeneo hayo
aliwaweze kufanya maandalizi ya ujenzi kwenye maeneo
waliotengewa .

0 comments:
Post a Comment