Na Walter Mguluchuma .
Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Reli TRL wameliagiza Shirika la Reli Tanzania kuhakikisha inapelela mabehewa ya mazigo ya kutosha katika Stesheni ya Mpanda kwa ajiri ya kusarisha mazao ya mahindi na mpunga uliokwama kusafirishwa kutoka Mpanda na kupelekwa kwenye maeneo yenye upungufu wa chakula .
Agizo hilo lilitolewa hapo jana na Wajumbe wa Bodi hiyo walipoitembelea stesheni ya Mpanda na kushitushwa na mrundikano wa mazao ya mahindi na mpunga yaliokwama kusafirishwa kutokana na upungufu wa mabehewa ya mazigo .
Mwenyekiti wa bodi ya TRL Prof John Kondoro alisema yapo baadhi ya maeneo hapa Nchini yana upungufu wa chakula hivyo ni lazima mazao yalio rundikana katika stesheni ya Mpanda kwa ajiri ya upungufu wa mabehewa ya mizigo yakasafirishwa haraka na kufika kwenye maeneo yanako safirishwa .
Alifafanua kuwa wao wajumbe wa bodi hawakuwa wanajua kama kuna mrundikana mkubwa wa kiasi hicho cha mazao ya mahindi na mpunga hivyo ziara yao ya siku moja imewasaidia kutambua tatizo hilo ambalo lipo ndani ya uwezo wa TRL .
Mkurugenzi Mkuu wa TRL Masanja Kadogosa aliwahakikishia wajumbe wa bodi hiyo kuwa tatizo hilo atalishughulikia na ndani ya kipindi cha wiki moja kuanzia sasa hakuta kuwa na mlundikano wa mazao kwenye stesheni hiyo ya Mpanda mazao yote yatakuwa yamesafirishwa .
Na limwagiza mkuu wa kitengo cha TRL anae husika na kusafirisha mizigo waliyekuwa nae kwenye ziara hiyo abaki Mpanda mpaka hapo mazao yaliorundikana kwenye stesheni yatakapokuwa yamesafirishwa yote .
Pia Mkurugenzi Mkuu huyo alisema TRL inatarajia kuongeza safari za treni ya abiria kutoka tatu kwa wii hadi nne kutoka Tabora hadi Mpanda kutokana na kuongezeka kwa iidadi ya wasafiri wakati huu wa kipindi cha kiangazi .
Aidha wanaangalia uwezekano wa kuleta behewa la daraja la kwanza la abiria endapo kama itaonekana kuna mahitaji ya abiria wa kutosha wanao hitaji kufafiri kwa daraja hilo la kwanza .
No comments:
Post a Comment