Na Walter Mguluchuma, Katavi.
Mbunge wa viti Maalumu wa Mkoa wa Katavi Anna Lupembe CCM ametoa msaada wa hundi ya Tshs milioni 5 kwa ajiri ya LETIC SACCOS ya wanawake ili kuiongezea nguvu Saccos hiyo ili wanachama wake waweze kujikomboa kiuchumi
Msaada huo wa hundi ulikabidhiwa hapo jana kwa Saccos hiyo na Katibu wa CCM wa Mkoa wa Katavi Kajoro Vyahoroka kwa niaba ya Mbunge wa viti maalumu na makabidhiano hayo yalifanyika katika viwanja vya CCM Mkoa wa Katavi .
Kajoro aliwaeleza akina mama hao kuwa fedha hizo wanaweza kuziona kuwa ni ndogo lakini endapo fedha hizo wakizitumia vizuri zitaweza kuwasaidia na kuweza kuongeza kipato chao .
Aliwasisitiza kuwa fedha wanazokuwa wamekopeshwa ni vizuri zikarejeshwa kwenye Saccos yao ili na watu wengine nao waweze kukopeshwa na kunufaika na fedha hizo .
Aliwataka viongozi wa SACCOS hiyo kujenga tabia ya kuwatembelea wanachama wao ili kuweza kujua changamoto wanazokabiliana nazo kwenye biashara zao na kuweza kuwapa ushauri .
Katibu wa SACCOS hiyo Mawazo Manso alieleza kuwa Saccos hiyo inadhaminiwa na Mbunge wa viti Maalumu Anna Lupembe ambae baada ya kuona Saccos hiyo inaanza kulega lega ameamua kuiongezea kiasi hicho cha fedha shilingi milioni tano .
Alisema mpaka sasa wapo jumla ya wanachama 75 ambapo hapo awali walikuwa 60 na wanachama 15 wamejiunga mwezi huu na mpaka sasa Mbunge huyo ameisha towa kiasi cha shilingi Milioni 45 kwani hapo awali alikuwa ameipatia Saccos hiyo kiasi cha shilingi milioni 40.
Alifafanua kabla ya kupewa fedha hizo akinamama hao wanaunda Saccos hiyo waliandaliwa mafunzo na Mbunge huyo ya ujasiliamali yaliofanyika kwa muda wa siku sita na walifundishwa na mkufunzi kutoka Dares salaam.
Mwenyekiti wa Saccos Maria Futakaba alisema wanaotunza familia ni akina mama hivyo endapo fedha wanazopewa watazitumia vizuri zitasaidia kwenye familia zao kwa kuweza kusomesha watoto na pia kuwa na familia yenye afya nzuri .
Aliwataka wanachama kurejesha fedha wanazo patiwa kwani wanao vunja chama ni wanachama wenyewe na wala si mtu mwingine .
No comments:
Post a Comment