*Lashindwa kufanya kazi saa 24
*Matarajio ya wananchi yatoweka
NA WALTER MGULUCHUMA, Katavi
ILIKUWA
ni Jumanne ya Januari 17 mwaka huu pale wananchi wa Manispaa ya Mpanda
na Mkoa wa Katavi kwa ujumla walipoyaona mapambazuko ya aina yake katika
sekta na huduma ya afya.
Sekta
hii muhimu katika maendeleo ya taifa, kwa miaka mingi imekuwa
ikikumbana na changamoto kadhaa karibu kila kona ya Tanzania, kubwa
ikiwa ni upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.
Jumanne
hiyo ya kukumbukwa ndio siku ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
alipozindua duka la serikali linalomilikiwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD)
lililopo katika Hopitali ya Manispaa ya Mpanda ambayo ndio
inayotumika kama Hospitali ya Mkoa wa Katavi.
Wananchi
waliohudhuria hafla hiyo waliifurahia hatua hiyo kutokana na ukweli
kwamba mbali na uhaba wa dawa na vifaa tiba kwa mikoa iliyopo pembezoni
mwa Tanzania, Katavi ni mmojawapo, tatizo jingine ni ukubwa wa bei za
dawa.
“Hili
duka la serikali litatuuzia dawa kwa bei tunayoimudu wengi tofauti na
maduka ya wafanyabiashara wengine,” alisikika akisema kwa matumaini
makubwa mmoja wa wananchi waliokuwapo siku hiyo.
Huenda
matarajio na matamanio hayo yakawa yameanza kufifia ndani ya miezi
minne tu tangu kufunguliwa kwa duka hilo. Ni nini sababu ya kupungua kwa
matumaini hayo?
Serikali
ya Awamu ya Tano kwa nia njema kabisa, inaendelea na ukaguzi na
ufuatiliaji wa vyeti vya kitaaluma kwa wafanyakazi wake kwenye sekta
mbalimbali, ikiwamo pia hii sekta nyeti ya afya.
“Hii
ni hospitali kubwa mkoani Katavi; ndio kimbilio letu na haistahili
kukosa dawa na vifaa tiba hata vile vya msingi kabisa, lakini bahati
mbaya hata bada ya kuwapo kwa dula la MSD, bado tunalazimika kununua
dawa kwa wafanyabiashara,” anasema Said Juma, Mkazi wa Kawajense mjini
hapa.
Juma
anasema Duka la MSD nalo lina matatizo yale yale yaliyopo hospitalini
hapo; halina dawa muhimu kwa magonjwa ya kawaida kabisa kwa wakazi wa
Mpanda!
“Shida
inakuwa kubwa zaidi nyakati za usiku kwani maduka mengi ya dawa huwa
yamefungwa. Kimbilio letu huwa ni Duka la Dawa la Mkasu lililo jirani na
hospitali. Hapo kila alfajiri utakuta watu walikuwa wakihitaji huduma
tangu usiku wa manane, wakisubiri lifunguliwe,” anasema na kuongeza kuwa
aghalabu nalo huwa halina baadhi ya dawa walizoandikiwa wagonjwa wengi.
Kukosekana
kwa dawa jirani na hospitali, kwa upande mwingine, ni neema kwa
waendesha bodaboda wenye kijiwe karibu na Hospitali ya Mkoa na mmoja
wao anasema:
“Watu
wengi huwa na haraka ya kununua dawa mbali na hospitali, maeneo ya
mjini. Hawa lazima wakodi bodaboda. Hii ndio huduma yetu kwa wananchi na
kwetu sisi ni kazi pia.”
Wakati wa uzinduzi wa duka hilo, iliahidiwa kuwa lingefanyakazi saa 24 likiwahudumia wakazi wa Mpanda na mikoa ya jirani.
“Duka
hili litamaliza tatizo la upungufu wa dawa katika hospitali hii, vituo
vya afya na zahanati za Mkoa wa Katavi. Serikali ina mikakati ya
kufungua maduka ya dawa kupitia MSD kwenye kila mkoa hapa nchini ili kuondoa tatizo la vifaa tiba na dawa na kuwapunguzia wananchi gharama za matibabu,” alisema Majaliwa.
Lakini
sasa duka hilo hufanyakazi kwa saa kadhaa tu kwa kuwa hulazimika
kufungwa nyakati za usiku kutokana na uhaba wa wafanyakazi.
Walau
wafamasia watatu waliokuwa wakihuduma dukani hapo wamekumbwa na zoazoa
ya vyeti feki na hivyo kuathiri huduma za duka hilo na kuongeza matatizo
zaidi juu ya upungufu uliopo wa dawa dukani hapo.
Wakati
wa uzinduzi Januari mwaka huu, Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurent
Bwanakunu, lengo la kufungua maduka katika mikoa saba nchini ni kusogeza huduma karibu na wananchi waweze kupata dawa bora na kwa bei nafuu.
Hata hivyo, ahadi hizo za Waziri Mkuu na Mkurugenzi wa MSD hazijafanikiwa kutatua tatizo la upungufu wa dawa mkoani Katavi.
Kwni
mpaka sasa dawa nyingi zimekuwa zikinunuliwa na wananchi kwenye
maduka ya Wafanya biahara wa mitaani kutokana na duka hilo la MSD
kutokuwa na dawa zenye mahitaji kwa wananchi.
Baadhi
ya wananchi wameanza kuingiwa na mashaka kuwa huenda ndani
zinazoletwa hapo ni zile ambazo sio mahitaji kwa wakazi wa
Mkoa wa Katavi .
0 comments:
Post a Comment