Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Watu wa tatu wamekufa hapo hapo bada ya gari waliliokuwa wakisafilia kugonga gema la ukuta wa barabara na kisha kupinduka huku likiwa limebeba magongo ya miti za mbao haina ya mkulungu .
Ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu wa tatu ilitokea hapo juzi majira ya saa tisa na nusu usiku huko katika eneo la Kijiji cha Kanoge Katika makazi ya wakimbizi ya Katumba Wilayani Mpanda .
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda alisema kuwa ajari hiyo ililihusisha gari lenye Namba za usajiri T880 BNX aina ya kenta lililokuwa likiendeshwa na dreva aliyejulikana kwa jina moja la Boni ambae ndie mmiliki wa gari hilo .
Alisema gari hilo lilikuwa likitokea Katumba katika makazi ya wakimbizi ya Katumba huku likiwa linaelekea Mpanda Mjini na lilikuwa limepakia mazao ya mistu magogo ya mti wa mkulungu .
Majina ya watu waliokufa hayaja julikana bado na mili ya marehemu hao watatu waliokufa kwenye ajari hiyo imehifadhiwa katika Hositali ya Manispaa ya Mpanda kwa ajiri ya kutambuliwa na ndugu zao.
Kamanda Nyanda alieleza kuwa chanzo cha ajari hiyo kilitokana na mwendo kasi wa wa dreva wa gari hilo hari ambayo ilisababisha dreva wa gari hilo kushindwa kuliumudu na kugonga gema na kisha kupinduka .
Alisema Dreva wa gari hili alikimbia mara baada ya kutokea kwa ajari hiyo na jeshi la Polisi linaendelea na msako wa kumsaka ili aweze kujibu mashitaka yanayomkabili .
Kamanda Nyanda ametowa wito kwa madreva kufuata sheria za usalama barabarani na wamiliki wa magari waache tabia ya kusafirisha mazao ya mistu muda wa usiku mazao ambayo yanakuwa wameyapata kwa njia ya nje ya utaratibu.
0 comments:
Post a Comment