Na Walter Mguluchuma.
Katavi .
Mwanafunzi wa darasa la pili shule ya Msingi Mnyamasi Kijiji cha Vikonge Kata ya Ntongwe Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Felista Oto Moses 9 amefariki Dunia baada ya kupigwa fimbo katika sehemu mbalimbali za mwili wake na mama yake mzaz ambae alikuwa amelewa pombe ya kienyeji.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda aliwaambia wandishi wa Habari jana kuwa tukio hilo lilitokea hapo juzi majira ya saa kumi na mbili jioni nyumbani kwa wazazi wa marehemu huyo Kijijini hapo.
Kamanda Nyanda alimtaja aliyempiga mtoto huyo hadi kufariki Dunia kuwa ni Maria Jackisoni 27 ambaeo ni mama mzazi wa marehemu huyo aliyekuwa akiishi nae nyumbani kwake na mumewe.
Alisema kabla ya tukio hilo mama wa marehemu wa mtoto huyo alikwenda kwenye klabu cha kuuza pombe za kienyeji aina ya komoni na kunywa pombe hiyo akiwa na jirani zake aliokuwa amefatana nao .
Maria Jackisoni baada ya kuwa amekunywa pombe na kutosheka aliwaaga wenzake kuwa anarudi nyumbani kwake kwa lengo kwenda la kuandaa chakula cha usiku cha familia yake .
Alipofika nyumbani alimwita marehemu na kisha alianza kumpiga katika sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kutumia fimbo lisha ya mtoto huyo kupiga mayowe ya kuomba msaasa kwa majirani lakini majirani hawakuweza kufika kwenye eneo hilo kufuatia kauli za hapo nyuma za mama wa mtoto huyo alikuwa akiwajibu walipkuwa wakimsihi asiwe anampiga mtoto huyo na mara zote alikuwa akiwajibu kuwa hakuna aliyemsaidia kumzaa mtoto huyo.
Baada ya kuwa amempiga mtoto huyo kwa muda mrefu mtoto huyo alianza kuishiwa nguvu na mama huyo hakujali aliendelea kumpiga tuu hadi alipofariki Dunia kutokana na kupingwa fimbo nyingi kupita kiasi na mama yake mazazi .
Alisema chanzo cha mama kumpiga mtoto huyo hadi kufa kulitokana na mama wa marehemu kumpiga mtoto huyo huku akiwa amelewa pombe kupita kiasi .
Mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi kwa ajiri ya mahojiano zaidi na mara baada ya uchunguzi kuwa umekamiliki atafikishwa mahakamani ili aweze kujibu mashitaka yanayo mkabili mtuhumiwa huyo .
0 comments:
Post a Comment