Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Wakazi wanao ishi katika Mkoa wa Katavi wametakiwa kuacha tabia ya kusafiri kwa kutumia usafiri wa Maroli kwani kwa sasa Mkoa huu unayo mabasi ya kutosha yanayofanya safari zake kwenda katika Mikoa mingine ya hapa Nchini.
Wito huu ulitoleewa hapo juzi na Afisa wa Mamlaka ya usafiri wa Nchi kavu na majini SUMATRA wa wa Mkoa wa Katavi Amani Mwakalebela wakati wa uzinduzi wa safari za mabasi ya Kampuni ya Adventure Connection yatakayo anza safari zake kutoka Mjini Mpanda Mkoani Katavi hadi Deres salaam uzinduzi huu wa safari ulifanyika katika stendi kuu ya mabasi yaendao Mikoani iliko katika Mtaa wa Mji Mwema mjini hapa .
Alisema kutokana na kuboreshwa kwa barabara za Mkoa huu kumefanya mwenye mabasi wahamasike na kuleta mabasi yao hivyo ni vema wakazi wa Mkoa huu wakasafiri kwa kwa mabasi badala ya kusafiri kwa maroli ambayo .
Mwakalebela aliwataka abiria waache tabia ya kuwashangilia madreva wanao endasha mabasi kwa kwendo kasi kwani kufanya hivyo wanahatarisha uhai wa maisha yao .
Awali kabla ya uzinduzi huo wa safari za mabasi ya kampuni ya Adventure wajumbe wa kamati ya usalama barabarani walitowa elimu kwa madreva pamoja na abiria .
Mwenyekiti wa usalama barabarani wa Mkoa wa Katavi Nassor Arfi aliwasisitiza wamiliki wa mabasi kutoza nauli zile ambazo zimepangwa na SUMATRA
Aliipongeza kampuni hiyo kwa kuzindua safari zake za kutoka Mpanda kuelekea Dares salaam kwani itakuwa ni mkombozi kwa wasafiri ambao walikuwa wakitumia siku mbili hadi tatu kuweza kufika Dares Salaam lakini sasa watakuwa wanatumia siku moja tuu.
Meneja wa Kampuni ya Adventure Nassor Ally alisema kuwa kampuni hiyo imejipinga na itaendelea kuboresha huduma kwa ajiri ya wateja wake kila wakati .
Alisema watakuwa wakifanya safari hizo mara tatu kwa wiki na basi zao zitakuwa zikipita katika Mikoa ya Tabora , Singida, Dodoma, Morogoro hadi Dares Salaam.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment