Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma.
Katavi
WAGANGA wa kiume wa tiba asili na tiba mbadala mkoani Katavi
wametakiwa kuacha mara moja tabia ya kufanya ngono na wanawake
wenye matatizo ya uzazi ambao hawajabahatika kupata watoto ili
waweze kupata ujauzito na kujifungua salama .
Rai hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi wa Tiba ya Asili kutoka
Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto , Dk
Paul Mhume wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja
yaliyowashirikisha waganga wa tiba asili na tiba mbadala kutoka
Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi .
Mafunzo hayo yalifunguliwa na na Katibu Tawala wa mkoa wa Katavi ,
Kamishina wa Polisi , Paulo Chagonja .
“ Wanawake ambao hawajabahatika kupata watoto kutokana na matatizo
ya uzazi wamekuwa wakikimbilia kwa waganga wa tiba ya asili kwa kuwa wanawaamini sana.…
wamekuwa wakiambiwa na waganga hao kuwa ili waweze kupata watoto
lazima wafanye nao ngono tena bila kutumia kinga hii
inahatarisha afya za wanawake hao kwani wanaweza kupata maambulizi
ya magonjwa yanayosababishwa na ngono zembe “ alieleza .
Aliongeza kuwa visa hivyo vinavyovyanywa na waganga hao kwa wateja
wao wa kike vimekuwa vikisababisha wanawake hao kupewa ujauzito na
waganga hao bila waume zao kufahamu .
Aliwatahadharisha waganga hao kuwa kwa kufanya hivyo wanajivunjia
heshima mbele ya jamii inayowazunguka .
Kwa upande wake Msajili wa Baraza la Tisa Asili na Tiba mbadala , Dk
Ruth Suza alisema kuwa baadhi ya waganga wa tiba asili na tiba
mbadala wamekuwa wakiwadanganya wateja wao kuwa ili watajirike
lazima kwanza wawabake binti zao wadogo kiendo ambacho ni kosa la
jinai .
“Lazima mzingitie miiko na maadili ya kazi yenu kwani wapo miongoni
mwenu wanaosababisha uvunjifu wa amani kwa kupiga ramli chonganishi
aghalabu husababisha mauaji “ alisisitiza
Aliwaonya waache tabia ya kuwaweka akina wajawazito nyumbani kwao
wakati ambapo hawawezi kuwazalisha badala yake watoe taarifa kwenye
vituo vinavyotoa huduma za afya ili waweze kupatia tiba sahihi na
kuepusha vifo vya wajawazito na watoto visivyo vya lazima .
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa KataviChagonja
aliwataka waganga hao wazingatie maadili kwa kuacha kupiga
ramli chonganishi pindi wanapokuwa wanawahudumia wateja wao .
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi , Dk Yahaya Hussein alisema
mkoa huo unaendelea na zoezi la kusajiri waganga wa tiba asili
tiba mbadala kupitia waratibu wa ngazi ya wilaya kwa
kushirikiana na uongozi wa waganga wa tiba asili .
Alisisitiza kuwa lengo la zoezi hilo ni kuhakikisha waganga wote
wa tiba asili na tiba mbadala wanafanya kazi zao kwa kufuata
kanuni na taratibu za Serikali
Alisema kuwa hadi sasa Mkoa wa Katavi
unao waganga wa Tiba asili na tiba mbadala 316 ambao wanaotambulika
na 165 wakiwa tayari wameisha sajiriwa .
0 comments:
Post a Comment